Kutoka
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Mji wa Geita, Zahara Michuzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Geita, John Paul Wanga
(aliyevaa kofia) wakimsikiliza Mtumishi wa Mamlaka, John Wanjala (kushoto)
baada ya kutembelea banda la Mamlaka kwa ajili ya kufahamu majukumu ya Mamlaka
na namna wanavyoweza kuwasaidia wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Mkoa wa
Geita hasa kwenye matumizi salama ya kemikali.
Mtumishi
wa Mamlaka, Eunice Mbata (kulia, picha ya kwanza) na Hadija Makurunge (kulia,
picha ya chini) wakiongea na wananchi wa Geita waliotembelea banda la Mamlaka
kwenye Maonesho ya
nne ya Teknolojia na Uwekezaii kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika
Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji, Bombambili mkoani Geita.
Watumishi
wa Mamlaka, Leah Kalinga (kushoto, picha ya kwanza) na Lowasa Kerika (kulia,
picha ya pili) wakiongea na wadau waliotembelea banda la Mamlaka katika
maonesho ya nne ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayofanyika
katika Kituo cha Uwekezaji (EPZ) kilichopo eneo la Bombambili mkoani Geita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...