KAMPUNI Ya Kiteknolojia ya Mawasilino Tanzania VODACOM Plc imeendelea na kasi ya kufikisha huduma za mtandao kidigitali kwa kuzindua awamu ya pili ya mpango wa upanuzi wa huduma za malipo ya kimataifa  kupitia kampeni mpya iitwayo 'Dunia Kijiji, Afrika Mashariki ni Yako.' ambapo wateja wanaweza kufanya malipo ya moja kwa moja kutoka M-Pesa  kwenda kwenye benki zote katika nchi za Afrika Mashariki za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar s Salaam Mkurugenzi wa huduma za M-Pesa kutoka Vodacom Epimack Mbeteni amesema uzinduzi huo ni ubunifu na uwezo mwingine mpya utakaowawezesha watanzania kutuma pesa na kutoka M-Pesa kwenda kwenye benki zote za Afrika Mashariki na kufanya ongezeko kubwa katika huduma zao za uhamishaji fedha kimataifa.

Amesema, Kampuni hiyo imekuwa ya kwanza kuanzisha huduma za kifedha kimtandao nchini na kujenga msingi imara wa kuendeleza upatikanaji wa huduma za kifedha kama vile malipo ya bili, akiba na mikopo pamoja na malipo ya biashara na mkakati wa huduma ya M-Pesa ni kuhakikisha inaongoza njia ya kuifikisha Tanzania katika jamii isiyotegemea pesa taslimu na kuwa na mfumo mpya wa huduma za kifedha kupitia menu ya *150*00#.

Mbeteni amesema, Katika huduma hiyo mpya inamletea  mtumiaji urahisi hasa kwa kuepukana na foleni katika mabenki na kutuma miamala, usalama wa fedha katika kufanikisha miamala jambo litakalochochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi ikiwemo biashara ndani ya ukanda wa Afrika.

Kampeni hiyo imelenga kuelimisha jamii ya juu ya huduma mpya pamoja na kushawishi wafanyabiashara na jamii kuanza kuitumia huduma hiyo mapema katika shuguli za kijamii, uchumi, malipo ya ada na matumizi ya kijamii.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa kampuni ya Thungs, Afrika Mashariki Joseph Njogu ambao wamekuwa wakishirikiana na kampuni ya  Terrapay katika kuhakikisha uimara wa mtandao wa kutuma pesa kwa njia ya mtandao amesema kuwa, huduma hiyo mpya ni fursa kwa watanzania kwa kutuma fedha nje ya mipaka kidigitali bila mipaka na kwa gharama nafuu kabisa kwa M-Pesa ambayo imekuwa ikienda mbali zaidi.

Mkurugenzi wa huduma za M-Pesa kutoka Vodacom Epimack Mbeteni akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya 'Dunia Kijiji, Afrika Mashariki ni Yako' ambayo zitawawezesha watumiaji wa huduma za M-Pesa kutuma pesa kwenye benki zote katika nchi  za ukanda wa Afrika Mashariki, Leo jijini Dar es Salaam.



Mkuu wa Kitengo cha malipo ya kimataifa kutoka benki ya Equity Patrice Kiiru akizungumza katika hafla hiyo na kuwataka watanzania kutumia fursa hiyo itakayoinua na kuchochea shughuli za kiuchumi na biashara ndani ya ukanda huo, Leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Terrapay kanda ya Afrika Mashariki Willie Kanyeki akizungumza wakati wa hafla hiyo na kuahidi huduma bora zenye ufanisi na gharama nafuu kwa watumiaji wa huduma hiyo, Leo jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Thungs, Afrika Mashariki Joseph Njogu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo na kuwataka watanzania kutumia fursa hiyo kupitia huduma za M-Pesa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...