Na Mwaandishi Wetu Mtwara

KATIKA Kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, wafanyakazi wa kiwanda cha Saruji Dangote Mkoani Mtwara leo wameungana na wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mtwara kupanda miti 1000 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza malengo ya  Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kuhifadhi na kulinda mazingira nchini.

Wafanyakazi hao wakiongozwa na Mkurungezi wa Uendeshaji wa Kiwanda cha Dangote,  Annadurai Appavoo walipanda miti hiyo katika eneo la Kiwanda hicho cha Dangote, eneo la hifadhi ya chanzo cha maji katika kijiji cha Mbuo na eneo la Shule ya Msingi ya Dunstan Kyobya iliyopo katika kijiji cha Hiari.

Akizungumza na wanahabari kuhusu zoezi hilo la kupanda miti, Meneja Mawasiliano wa Kiwanda Cha Dangote Rachael Singo amesema zoezi la upandaji miti limelenga kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania katika kulinda na kuhifadhi mazingira, kuhamasisha wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti kwa ajili ya kukabiliana na changmoto ya mabadiliko ya tabia nchi.

“Dangote kama Taasisi duniani kote wiki hii ni muhimu sana kwetu, tunaungana na Umoja wa Mataifa kutekeleza malengo endelevu 17 ambapo kitaifa sisi Dangote Tanzania tunatekeleza malengo matatu ambapo moja wapo ni kutatua changmoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi,” amesema.

Singo amesema watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kukata miti sababu ambayo imekuwa ikipelekea kuwepo kwa athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia  nchi ambazo huathiri mazingira na maisha ya watu, ikiwa ni pamoja na kukosa hewa safi.

“Kwa sababu hiyo tunahamisisha watanzania kupanda miti kwa wingi. Mtu akikata mti mmoja anatakiwa kupanda miti angalau mitano,” amesema na kuongeza kuwa aina ya miti iliyopandwa na wafanyakazi hao ni pamoja na miti ya kivuli, matunda na maua.

Abdullhali Mohammed Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuo, ameshukuru uongozi wa Kiwanda hicho kwa kupanda miti katika kijiji hicho akisema miti hiyo itasaidia katika kulinda mazingira na chanzo cha maji kilichopo katika eneo la kijiji.

“Kwanza ninashukuru Dangote kwa zoezi hili la upandaji miti maeneo ya kijiji changu hii itatusaidia kuhifadhi vyanzo vyetu vya maji ili visiweze kukauka, vyanzo vya maji vikikauka ni hasara kwa jamii nzima, na kwa bahati nzuri vyanzo hivi vinanywesha vijiji visivyopungua kumi na nne Mtwara DC,” amesema na kuomba uongozi wa Kiwanda hicho kufikiria kupanda miti zaidi katika  eneo huku akiahidi kutunza na kulinda miti hiyo ili ikue kwa faida ya jamii na vizazi vijavyo.

Afisa Mazingira wa Halmashuri ya Mtwara Ben Salma (Kati) pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Mbuo wakipanda mti katika eneo la Hifadhi ya Chanzo cha Maji katika Kijiji cha Mbuo.

Wafakazi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichop Mkoani Mtwara wakipanda miti kuadhimisha Wiki ya Utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa kuunga mkono kuhudi za Serikali katika kutekeleza lengo la kuhifadhi na kulinda mazingira nchini

 
Mratibu wa wiki ya Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, Dangote Tanzania Abayomi Awofodu (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbuo Abdullah Mohammed wakipanda mti katika eneo la Hifadhi la chanzo cha Maji Mbuo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...