Na Mwandishi Wetu
 
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, amepongeza ushirikiano wa Shirika la Vijana (Tayoa) kwa serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Ameyasema hayo leo Septemba 16,2021 jijini Dodoma alipotembelea banda la Shirika hilo na kuelezwa kazi zinazofanywa na shirika hilo ikiwemo kusambaza kondom na makasha ya kusambazia mipira hiyo vijijini.

Maonyesho hayo yamefanyika pembeni ya mkutano mkuu wa mwaka uliowashirikisha waganga wakuu wa mikoa yote nchini na wa halmashauri na kufanyika kweye ukumbi wa Jakaya Kikwete.

Gwajima amesema huduma ya usambazaji mipira ya kiume ni muhimu sana hivyo shirika hilo ni vyema likaendelea kusambaza ili kuwafikia vijana wengi nchini hali ambayo itasaidia kwa kiwanggo kikubwa kupambana na ugonjwa huo hatari.

“Nawashukuru sana Tayoa mmekuwa mkishirikiana vyema na serikali na endeleeni kuhakikisha huduma zenu za kusambaza mipira ya kiume zinawafikia watu wengi zaidi,” alisema Waziri Gwajima

Akizungumza kwenye mkutano huo, Waziri Gwajima amefurahishwa na kauli mbiu ya mkutano huo inayosema ustahimilivu wa mifumo ya afya katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID 19.

Amesema pamoja na changamoto zilizopo waganga wakuu wa mikoa na halmashauri wameendelea kutumia weledi wao kutumikia jamii katika mapambano ya ugonjwa huo.

“Hili ni jambo la kizalendo hongereni na nichukue nafasi hii kuwaelekeza viongozi wote kuhamasisha wananchi kwenda kupata chanjo ya COVID 19 kwani chanjo hiyo ni salama,” alisema
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, akionyesha kondom aina ya safari inayosambazwa na Shirika la Vijana Nchini (Tayoa) kwenye maonyesho yaliyofanyika pembeni ya mkutano wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tayoa, Peter Masika kuhusu makasha ya kusambazia kondo na kondom aina yaa safari zinazosambazwa na shirika hilo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, akibonyeza mashine kwaajili ya kutoa kondom aina ya safari inayosambazwa na shirika la vijana nchini Tayoa wakati wa maonyesho yaliyofanyika pembeni ya mkutano wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Tayoa Peter Masika akimweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima kuhusu makasha ya kusambazia kondom kwenye maonyesho yaliyofanyika mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...