Waziri wa Maji Jumaa Aweso amezindua Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Dawasa) leo Ijumaa Septemba 17, 2021 na kuwataka wajumbe wakiongozwa na Mwenyekiti wao wasiwe na bodi ya makaratasi bali watembelee miradi ili kuweza kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kuzindua bodi hiyo Waziri Aweso amesema ikifanya kazi kwa ufanisi itaweza kuisimamia vyema menejimenti na kuwezesha kufikiwa malengo ya mamlaka hiyo hasa kwa kutembelea  miradi na kufuatilia utekelezaji wake ili lengo la Serikali la kuwafikishia wananchi Maji safi na salama litimie.

“‘Nendeni mkasimamie menejimenti, msiwe bodi ya vikao, DAWASA  inafanya kazi nzuri nendeni mkahakikishe kazi hiyo inaendelea na kuleta matokeo chanya zaidi ili iwe mfano wa kuigwa kwa Mamlaka nyingine za maji,” amesema Aweso.

Pia Aweso aliwakumbusha wakurugenzi wa mamlaka nyingine za Maji hapa nchi kuiga mfano wa DAWASA na kufanikisha lengo la kumtua mama ndoo kichwani na kuwasisitiza waje kujifunza kupitia utendaji kazi wa Mamlaka hiyo iliwaweze kufikia malengo waliyojiwekea.

“Kazi kubwa inafanyika na tunaiona sio vibaya kwa mamlaka nyingine kuja kujifunza hapa na Dawasa isiridhike izidi kufikisha maeneo ya pembezoni,”. Alisema Aweso

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja  amemshukuru Waziri wa Maji Jumaa Aweso kwa kuchagua Bodi nzuri mara baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange.

Amesema kazi iliyofanyika DAWASA kwa miaka mitatu ni kubwa sana chini ya Bodi iliyomaliza muda wake ikiwemo ya kuunganisha DAWASA na DAWASCO.

Amesema kwa kipindi kifupi sana DAWASA waliweza kupanua huduma zake ambapo mpaka sasa inahudumia takribani wananchi wapatao  milioni tisa kutoka mkoa wa Dar Es Salaam, Wilaya ya Bagamoyo, Mkuranga, Kihaba na Sehemu ndogo ya Tanga pamoja na sehemu ndogo ya Morogoro.

“Kupitia bodi hiyo iliyomaliza Muda wake DAWASA wameweza kuyakabiri maeneo sugu ambayo ni Segerea, Kinyerezi, Kipawa, Ukonga, Goba, Mvumuni, Salasala, Madale, Kwamsuguli pamoja Gongo la Mboto”. Alisema Luhemeja

Akizungumza kwa niaba ya bodi hiyo Mwenyekiti  Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange amesema watakahakikisha miradi yote inatekelezwa chini ya mamlaka hiyo na watahakikisha wanatembelea miradi yote na kuisimamia DAWASA ili kuweza kufikia lengo la kumtua mama ndoo kichwani.

Pia Waziri wa Maji Jumaa Aweso alitembelea na kujionea uendeshaji wa Kituo cha TEHAMA cha kukusanya Taarifa  za Mamlaka hiyo kabla ya kuzindua Bodi mpya ya DAWASA itakayodumu kwa Miaka mitatu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitolea ufafanuzi kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na viongozi mbalimbali kuhusu uendeshaji wa Kituo cha TEHAMA cha kukusanya  Taarifa za Mamlaka hiyo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Bodi mpya ya DAWASA

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso(kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma wakizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) leo jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso(kulia) akikabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso(kulia) akikabidhi vitendea kazi Katibu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja mara baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso(kulia) akikabidhi vitendea kazi kwa baadhi ya wajumbe wa Bodi ya DAWASA mara baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na Wajumbe wa Bodi wapya na wafanyakazi wa DAWASA pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA pamoja na kuwapatia vitendea kazi kwa kila mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa  Wizara  ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akizungumzia namna Serikali ilivyojipanga kusimamia mamlaka za Maji kuweza kutekeleza Miradi mikubwa pamoja na midogo ya maji wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa ufafanuzi kuhusu Bodi iliyomaliza muda wake ilivyofanya kazi kwa miaka mitatu chini ya Wenyekiti wake Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma akizungumza namana walivyojipanga kuweza kuzisimamia Mamlaka za Maji hapa nchini ikiwemo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ili kuweza kufanikisha upatikanaji wa Maji kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe Mpya wa Bodi ya DAWASA,  Kate Kamba akizungumza kuhusu namna Ilani ya Chama cha CCM inavyotaka wananchi wapatiwe maji safi na salama pamoja na kumshukuru Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa kumteua kuwa mjumbe wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi, wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)na wagei waalikwa wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimtambulisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange anayeendelea tena kwa miaka mitatu mingine leo wakati wa kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna alivyofurahishwa na utendaji wa DAWASA mara baada ya kutembelea na kupata maelezo ya Kituo cha TEHAMA cha kukusanya  Taarifa za Mamlaka. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso na wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza jambo mara baada ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA kuzinduliwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso itakayodumu kwa miaka mitatu.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga  , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA  Jeneral Mstaafu Davis Mwamunyange, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa  kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Maji.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga  , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA  Jeneral Mstaafu Davis Mwamunyange, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa  kwenye picha ya pamoja na wakuu wa wilaya ya Kisarawe na Bagamoyo mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Maji.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga  , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA  Jeneral Mstaafu Davis Mwamunyange, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa  kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa DAWASA baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Maji.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga  , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA  Jeneral Mstaafu Davis Mwamunyange, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa  kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka za maji za mikoa mingine mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Maji.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga  , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA  Jeneral Mstaafu Davis Mwamunyange, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa  kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Mamlaka nyingine pamoja na mashirika mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Maji.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga  , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA  Jeneral Mstaafu Davis Mwamunyange, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa  kwenye picha ya pamoja na Meneja wa mikoa ya DAWASA mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Maji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...