Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KOCHA Mkuu wa Young Africans SC, Nasreddine Nabi amesema kuwa Kikosi chake kinahitaji muda ili kupata matokeo bora uwanjani, kutokana na usajili na ujio wa Wachezaji wengi wapya katika Kikosi hicho msimu huu wa mashindano.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kocha Nabi amesema Yanga SC ina Wachezaji 28 bora waliosajiliwa kwa umakini kushirikiana baina ya Viongozi wa Klabu hiyo, Wadhamini wake GSM. Amesema Mashabiki wa Soka nchini wanatakiwa kuwa na subira ili kutengeneza muunganiko wa Wachezaji hao.

Pia ameeleza kuwa anaamini Yanga SC itakuwa bora Tanzania na Afrika kwa ujumla kutokana na Wachezaji wa viwango vya juu waliosajiliwa msimu huu kikosini hapo huku akiahidi furaha kwa Mashabiki wa Soka nchini kwa ubora wa Yanga SC baada ya kipindi hicho cha mpito.

“Nawahakikishia zaidi ya asilimia 200, Young Africans SC itakuwa timu bora Tanzania na Afrika kwa ujumla kutokana na usajili makini uliofanywa na Viongozi, Wadhamini wa Yanga SC”, ameeleza Nabi.

Kuhusu mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC, Kocha Nabi amesema ana furaha kuwa sehemu ya Makocha wawili watakaosimama kwenye Mabenchi ya ufundi kuongoza timu zao katika mtanange huo.

“Tangu turudi kutoka nchini Nigeria tutolewe kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Wachezaji waendelea kujiandaa na mchezo huo wa Watani wa Jadi huku tukijua utakuwa mchezo wa ushindani pande zote mbili. Tunajua Mashabiki Wetu wanataka ushindi na kufurahi pia”, amesema Kocha Nabi.

Wachezaji majeruhi Balama Mapinduzi, Yassin Mustafa Kocha huyo amesema wamekaa nje muda mrefu hivyo wanaanza mazoezi taratibu ili kupata ubora (fitness) kutokana na kukaa muda mrefu nje kuuguza majeruhi hayo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...