Na Humphrey Shao, Michuzi Tv Chanika

Wadada zaidi ya 32 wamepatiwa Mafunzo kuhusu madhara ya rushwa ya ngono kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa mradi wa Sauti ya Wana Jamii kipunguni

Akizungumza na Michuzi Tv mnufaika huyo Ratifa Mussa Amesema kuwa amefanikiwa kuwafikia weza akina Dada 32 tangu alipopata Elimu hiyo kutoka kwa tasisi ya Sauti ya Jamii kipunguni.

"Mimi ni mmoja wa wanufaika wa mradi wa kuzuia rushwa ya ngono ambao umefadhiliwa na Women Fund  kupitia sauti ya Wana jamii kipunguni hivyo nimeona niendelee kutoa Elimu hii kwa Wakazi wenzangu wa chanika  ili waweze kunufaika" Amesema Ratifa.

Ameongeza kuwa Ndoto yake ilikuwa ni kutoa hii elimu kwani yeye ni muathirika wa rushwa ya ngono ila kabla ya mafunzo hakujua aanzie wapi hivyo kwa kupata Mafunzo haya yamempa Mwanga na kuwasaidia wengine.

Ametaja kuwa wasichana wengi waliopo maeneo ya pembezoni hawana uelewa Mpana Jinsi ya kupambana na rushwa ya ngono, lakini kupitia sauti ya Wana Jamii kipunguni tumefanikiwa kupata elimu hiyo ambayo pia tuaitumia kuwasaidia akina dada wengine.

Kwa upande wake Mkufunzi kutoka sauti ya Wana Jamii kipunguni Selemani Bishagazi  amesema Ratifa ni mmoja wa akina Dada ambao wameweza kuwasaidia wakazi wa Chanika mara baada kupata Mafunzo.

Bishagazi ametaja kuwa mara ya kwanza Ratifa aliweza kuwafikia wadada 21 na mara ya pili amewafikia wadada 11 hivyo kuwa na mafanikio'' ya kuwasaidia wadada 32 mpaka sasa..

Mmoja wa Wanufaika wa Mafunzo ya madhara ya rushwa ya ngono Ratifa Mussa akizungumza na kundi la wasichana amabo amewakusanya kupata elimu.
Bi Ratifa Mussa akizungumza na Baadhi ya watu ambao wametoa mikataba kwa wadada wa Kazi.
Mkufunzi kutoka sauti ya Wana Jamii kipunguni Selemani Bishagazi akitoa maelekezo  kwa Ratifa Mussa bambaye ameandaa Mafunzo kwa wasichana zaidi ya 32


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...