MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, kutumikia kifungo cha miezi sita nje baada ya kupatikana na hatia ya kosa la matumizi mabaya ya ofisi.

Aidha mahakama imemuachia huru Godfrey Nyange  maarufu kama Kaburu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Hukumu hiyo imesomwa leo Oktoba 28,2021 na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba ambaye amesema hakuna ubishi wowote kuwq, USD 300,000 zilikuwa zimeingizwa kwenye akaunti ya Klabu ya Simba kupitia benki ya CRDB ambayo ni mauzo ya mchezaji Emanuel Okwi

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema upande wa mashtaka wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa Aveva alitenda kosa la matumizi mabaya ya ofisi  na mahakama imemkuta na hatia na kumuhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita nje.

 Aveva amekutwa na hatia Kwa kutumia nafasi yake vibaya kwa kuingiza ongoza fedha hizo kwenye akaunti binafsi ingawa hakuna wizi uliofanyika amesema Simba.

Amesema baada ya kuingia kwenye  akaunti hiyo inaonyesha kwamba kamati tendaji ya  klabu ya simba ilielekeza itolewe fedha hiyo kwenye akaunti ya Simba ili itumike kwenye uwanja wa Bunju kwa kujenge nyasi bandia lakini haikufanyika hivyo na badala yake zilienda kwenye akaunti binafsi ya Aveva.


Baada ya maelezo hayo Wakili wa serikali Fatima Waziri alidai hawana kumbukumbu ya makosa ya jinai yaliyotendwa na mshtakiwa huyo hivyo naiomba mahakama itoe adhabu Kali ili iwe fundishi kwake na kwa wengine wanaotumia madaraka ya ofisi vibaya.

Akijiteteta Aveva, kupitia wakili wake, Kuge Wabeya ameieleza mahakama kuwa mteja wake ni mkosaji wa mara ya kwanza lakini pia ni mgonjwa amekuwa akihutdhuria kliniki mara tatu kwa wiki na pia ana familia inayomtegemea.

"Naiomba mahakama itoe adhabu nafuu itakayomuwesha Aveva kuhudhulia kliniki kwa wakati wakati akiwa "amedai Wabeya.

Hakimu Simba amesema kutokana na mazingira amezingatia hoja za pande zote mbili kuwa mtuhumiwa amekaa mahabusu Kwa muda mrefu mpaka pale mahakama ilipoona kosa la utakatulishaji haijadhibitisha.

"Kumpeleka gerezani Kwa maana kumfunga haitasaidia chochote kwani watakuwa wamemfunga mgonjwa ambaye utakuwa imesababisha usumbufu siyo Kwa mshtakiwa Bali hata magereza na jamii Kwa ujumla....na hata ukimpiga faini kubwa  bado haitasaidia chochote kwani asipolipa atalazimika kupelekwa gerezani hivyo adhabu pekee inayomfaa mahakama imeona atumikie kifungo cha nje miezi Sita na asifanye kosa lolote,"amesema simba

Aveva na Kaburu walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29, 2017 na kusomewa mashtaka kumi ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kughushi nyaraka zilizoonesha kuwa klabu hiyo ilikuwa ikililipa mkopo wa dola za Marekani 300,000 kwenye akaunti ya Aveva na utakatishaji haramu wa fedha.

Kesi hiyo iliendelea kutajwa washtakiwa hao wakiwa mahabusu hadi ilipofika Septemba 19, 2019 walipoandika barua ya kukiri na kuomba kumaliza kesi hiyo kwa njia ya majadiliano na Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) lakini upande wa mashtaka uliieleza mahakama kuwa walikuwa katika mchakato wa kuwafutia mashtaka ya utakatishaji fedha washtakiwa hao na ikalazimu majadiliano hayo kusubiri, hata hivyo hayakufanyika.

Oktoba 11, 2019 washtakiwa hao walifutiwa mashtaka ya utakatishaji fedha haramu na kupewa dhamana 

Katika kesi hiyo inadaiwa,  Aveva na Kaburu walikula njama ya kutenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka na pia walidaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha USD 300,000 kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays.

Katika shtaka la tatu, Aveva walidaiwa kwa pamoja kughushi nyaraka zilizoonesha kuwa Simba ilikuwa inalipa mkopo wa kiasi hicho cha fedha kwa Aveva jambo ambalo walijua kuwa si kweli.

Pia Aveva anadaiwa kutoa nyaraka za uongo kwa benki ya CRDB akionesha klabu ya ya Simba wanalipa mkopo huo.

Aveva anadaiwa kuwa katika Benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 187,817 wakati akijua zimetokana na kosa la kughushi nyaraka.

Katika shtaka la sita, Kaburu alidaiwa kumsaidia Aveva kujipatia kiasi hicho cha fedha kutoka kwenye akaunti klabu ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na kughushi nyaraka.

Pia walidaiwa kughushi hati ya malipo ya kibiashara wakionesha kwamba klabu ya Simba ilinunua nyasi bandia kwa gharama ya dola za Marekani 40,577 huku wakijua kwamba siyo kweli.

Katika shtaka la nane, Aveva anadaiwa kuwasilisha hati ya malipo ya kibiashara ya uongo  kwa Levison Kasulwa  kwa madhumuni ya kuonesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya USD 40,577 huku shtaka la tisa ilidaiwa washtakiwa hao waliwasilisha nyaraka za uongo kuonesha kuwa Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya dola za Marekani 40,577.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...