Na Bashir Nkoromo, Tegeta.

Baba Halisi wa Uzao jana aliwabariki Waandishi wa habari zaidi ya 50, waliohudhuria Ibada Maalum ya Kuwabariki Waandishi hao, iliyoandaliwa na Kanisa Halisi la Mungu Baba Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuwabariki Waandishi hao kutoka vyombo mbalimbali vya Habari, Baba Halisi alifanya shukrani (maombi) Maalum ya kumuinua Rais Samia Suluhu Hassan na Wasaidizi wake; Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine wote wa Serikali na Jamii kwa jumla.

"Maovu yote hutokana na Mamlaka, hivyo tunawainua (kuwaombea) viongozi wote wa Taifa letu ili Mungu Baba awalinde na kila ovu, wabarikiwe na kuwa huru katika utendaji wao, wafanye kazi zao kwa bidii na maarifa ili Tanzania iendelee kuwa na amani na utulivu na kuinuka zaidi kiuchumi na Kijamii", alisema Baba Halisi katika Ibada hiyo Maalum ambayo ilihudhuriwa pia na mamia ya Uzao (waumini wa Kanisa hilo).

Katika kuwabariki, Baba Halisi wa Uzao aliwaita Waandishi wa habari hao kusimama katika eneo Maalum mbele yake, baada ya kufika wakiwa kwenye sura za furaha alianza kuwafanyia maombi (shukrani) aliyosema kuanzia baada ya Ibada hiyo watakuwa wamepata Baraka za Mungu Baba ikiwemo kutochukiwa tena na jamii kwa ajili ya kazi zao na kufanya kazi zao za uandishi zikiwemo za kijamii, Biashara, siasa na Burudani kwa weledi na bila kubagua.

Maombi hayo Baba Halisi wa uzao aliyahitimisha kwa kuwanywesha kila mmoja 'Damu safi' (maji yaliyobarikiwa) na kisha kuagana nao kwa kuamuru Makuhani wa Kanisa hilo kuwapatia soda waandishi hao na wote walioshiriki kwenye Ibada hiyo Maalum wanywe kabla ya kuondoka.

"Nimefurahi sana kuwaona hawa wanangu (waandishi), basi Makuhani wapatieni soda wote, na Uzao wote waliomo humu wanywe soda, tufurahie sherehe hii kubwa", akasema Baba Halisi wa Uzao kabla ya kufunga rasmi Ibada hiyo Maalum.

Baba Halisi wa Uzao akiwafanyia shukrani (maombi) ya Kuwabariki Waandishi wa habari katika Ibada Maalum ya Kuwabariki Wanahabari hao iliyofanyika jana, Makao Makuu ya Kanisa Halisi la Mungu Baba, Tegeta jijini Dar es Salaam.
Baba Halisi wa Uzao akiendelea kuwafanyia shukrani (maombi) ya Kuwabariki Waandishi wa habari katika Ibada hiyo Maalum ya Kuwabariki Waandishi wa Habari.
Waandishi wa Habari wakiwa wamesimama kwa utulivu mbele ya Baba Halisi wa Uzao wakati akiwafanyika shukrani (maombi) hayo ya Kuwabariki.


Kisha Baba Halisi wa Uzao akawanywesha kila mmoja Damu Safi (Maji yaliyoyabarikiwa)

👇
PICHA MBALIMBALI ZA IBADA LIVYOKUWA👇





















Huyu ni Mama Halisi wa Uzao akiwa katika shamrashamra za kufurahia Ibada hiyo ya Kuwabariki Waandishi wa Habari, iliyofanyika jana katika Kanisa Halisi la Mungu Baba, Tegeta, Dar es Salaam. ©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...