Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui ( wa pili kulia) akifuatilia majadiliano wa sekta ya kilimo hai ambao wamekutana katika Mkutano Mkuu wa pili wa kilimo hai uliofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili.Wengine katika picha ni wawakilishi wa mataifa mbalimbali walioshiriki mkutano huo.

Baadhi ya wadau wa kilimo hai wakiandika taarifa muhimu kuhusu kilimo hicho wakati viongozi wa serikali na wadau wa kilimo hicho wakitoa michango yao ya namna gani kilimo hai kitaendelea kupewa kipaumbele.






Na Said Mwishehe,Michuzi TV

BALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesena Serikali ya Tanzania kwa sasa inaandika mkakati wa kitaifa ambao ni hatua kubwa kwa nchi hiyo kuongeza harakati za kilimo huku akieleza jamii za kiraia zina jukumu la msingi katika kukuza agroecology huku akiahidi kutoa kila aina ya msaada kufanikisha kilimo hai nchini.

Amesisitiza hawawezi kuifanya peke yao na kwamba Serikali ya Tanzania inadhihirisha kuwa mkutano wa wadau wa kilimo hai nchini kuona. Umuhimu kwa upanuzi wa sekta ya kilimo.

Akizungumza wakati wa majadiliano yaliyojikita kuangalia hatua za kuchukua kuimarisha kilimo hai na kushirikisha wadau wa kilimo hai katika mkutano huo uliofanyika Mkoa wa Dodoma ,Balozo Hajiloui amesema kwanza amefufahi kuona maofisa wa serikali na wadau wengine wa kijadili kuboresha kilimo hicho.

"Nimefurahi sana kusimama hapa leo, pamoja na maofisa wa Tanzania, washirika wa maendeleo, UN na wawakilishi wa asasi za kiraia, wakulima, na wanafunzi katika mkutano wa pili wa kitaifa wa kilimo hai wa mazingira. Hii inamaanisha mengi. Mnamo mwaka wa 2019, mkutano wa kwanza wa kitaifa ulifanyika Dodoma, kwa msaada mkubwa kutoka Ufaransa,"amesema.

Amefafanua katika mkutano huo ulioshirikisha wadau wa kilimo zaidi ya 400 ,Balozi huyowa Ufaransa nchini amesema"Leo, nataka kuangazia ukuaji na uwekaji taasisi kwa harakati za kikaboni nchini Tanzania".

Ameongeza kwamba katika pato la Taifa la Tanzania kilimo kinachangia asilimia 26.7 wakati katika ajira kinachangia asilimia 65 ya ajira za Watanzania ,pia kilimo ni chanzo cha uzalishaji wa GHG ulimwenguni kwa asilimia 24 mwezi uliopita.

Mwezi uliopita, Rais wa nchi ya Ufaransa aliitisha mkutano wa kilele wa mfumo wa chakula wa UN ambapo Ufaransa ilikuwa ikiongoza muungano kuhusu kilimo.

"Nchi yangu inasaidia agroecology kwa maono yake ya muda mrefu, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa."

Balozi Hajlaoui ameeleza wakati wa miongo kadhaa tangu 1970, Wakulima wa Ufaransa walikuwa wakifanya Kilimo na walitumia dawa nyingi za wadudu wakiharibu mchanga na maji.

Amesema athari hizo kwa mazingira na afya ziko juu sana katika maeneo mengi huko Ufaransa."Naweza kunukuu mfano tu: katika Kisiwa cha Ufaransa cha West Indies kinachoitwa Guadeloupe na Martinique, leo asilimia 99 ya idadi ya watu imechafuliwa na dawa ya wadudu iitwayo Chlordecone.

Amesema hiyo imechangia kuongezeka kwa Kiwango cha saratani pamoja na athari nyingine nyingi na hivyo kuifanya Serikali ya Ufaransa kuunda kikosi kazi kusaidia watu wa kifedha na kulipia matibabu yote.

Amesema baada ya miongo kadhaa, mnamo mwaka 2012 Rais Macron alibadilisha kabisa mkakati wa kitaifa na kujenga sera ya kugeuza kilimo cha awaida kuwa Organic.

''Katika miaka 10 iliyopita, Serikali ya Ufaransa ilibadilisha mkakati: Rais Macron alisema: "

Nchi yangu inasaidia agroecology kwa sababu inachochea uchumi wa ndani na wa kimataifa na masoko.Mahitaji ya bidhaa za kikaboni yanakua ulimwenguni kote.

"Kwa miaka miwili iliyopita, tunaweza kusisitiza ufunguzi wa maduka, Zanzibar na katika Bara kuuza bidhaa za kikaboni, kujibu mahitaji yanayoongezeka na kwasababu hizi zote, tunapaswa kudumisha harakati hizi zinazoongezeka, haswa hapa Tanzania,"amesema.

Amesisitiza kuwa Ufaransa itaendelea kusaidia Serikali ya Tanzania na Jumuiya za Kiraia katika kutekeleza miradi miwili ,wa kwanza katika mwaka 2019-2020 iliyogharimu kiasi cha fedha 900 000 000 € iliyotekelezwa na Swissaid, TOAM, SAT ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa.Mradi huo unafuatwa na mradi mpya wa miaka 2 wa 600 000 € kwa Bara na Zanzibar.

"Shirika la Maendeleo la Ufaransa linajadiliana na TADB ili kuanzisha mpango unaofadhiliwa na Mkopo ukilenga Wakulima Wadogo kukuza Kilimo Kilichostahimili.Nitumie mkutano huu muhimu kumpongeza na kumshukuru Bingwa wa Kilimo cha Kilimo hai na kama Mkurugenzi wa NGO wa Janet Maro, ambaye alialikwa na Ubalozi wa Ufaransa jijini Nairobi kwa Mkutano wa Sayari Moja mwaka 2019.

"Napenda kumshukuru kwa kujitolea kwake kwa nguvu, Mwatima Juma, mkurugenzi wa PPIZ, NGO isiyo ya kiserikali ya Zanzibar naye alihudhuria Mkutano wa mwisho wa Dunia wa Kikaboni huko Ufaransa Septemba mwaka huu,

Nilisikia kwamba Waziri wa Kilimo akielezea mikakati ya kuimarisha na kuongeza uzalishaji wa Organic na ataunda Idara iliyojitolea,"amesema Balozi Hajlaoui.

Aidha ameahidi mbele ya wadau wa kilimo hicho na viongozi wa Serikali walioshiriki majadiliano wakati wa mkutano huo kuwa atatoa kila aina ya msaada wake kwa Serikali ili kufanikisha ndoto hiyo."Timu yangu itafanya kazi kwa karibu na Serikali ikiwa kikosi kazi kitaundwa ili Kujiunga na juhudi za Watawala, Wahisani, Asasi za Kiraia na Sekta Binafsi, Ufaransa itakuwa kwenye Bodi''

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...