Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mkoani Kagera Mhe. Innocent Bashungwa amesema hatua ya Serikali kutoa kiasi cha shilingi Bilioni nne na milioni 900 kwa ajili ya maenedeleo Wilayani Karagwe itasaidia kuwezesha maenedeleo tamaniwa katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika jimbo lake.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari saa chache mara ya baada ya kuapishwa kushika wadhifa wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mara nyingine Ikulu jijini Dar Es Salaam.

Kauli ya waziri Bashungwa inakuja ikiwa ni siku chache Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe itoe tangazo la wazi kuwahabarisha wananchi juu ya kiasi cha fedha cha shilingi Bilioni 4, 983, 841, 905.87, kilichotolewa na Serikali kwa halimshauri hiyo kwa mwezi oktoba kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na uendeshaji wa ofisi.

Waziri Bashungwa amekaliliwa akisema "Kiu ya watanzania ni maendeleo na hakika kwa kasi hii ya kupeleka maendeleo kwenye kata zote nchini, sisi Karagwe tunaungana na Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Watanzania wote tukisema mama anaupiga mwingi"

Pamoja na mambo mengine kiasi hicho cha fedha kilichotolewa kitatumika kugharamia ujenzi wa madarasa 80 ya shule za sekondari, madarasa matano katika shule shikizi za msingi, ujenzi wa nyumba ya mtumishi na chumba cha ICU katika hospitali ya Wilaya Karagwe pamoja na kugharamia mitihani ya darasa la Saba, kidato cha pili na cha nne.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Karagwe Michael Nzyungu Oktoba 22, 2021, fedha hizo ni ruzuku ya maendeleo na matumizi ya kawaida kutoka Serikali kuu na wahisani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...