Na Munir Shemweta, WANMM UYUI

Serikali imetoa sehemu ya ardhi ya hifadhi ya Mto Igombe (Igombe River) kwa ajili ya wananchi wa vijiji 12 vilivyopo kwenye wilaya ya Uyui mkoani Tabora.

Utoaji sehemu ya ardhi hiyo ni muendelezo wa hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anawabakisha wananchi walioingia kwenye mgogoro wa muda mrefu na serikali kwa kuvamia sehemu ya maeneo ya hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba na pembezoni mwa Maeneo Chepechepe (Ardhi oevu).

Baadhi ya vijiji vilivyonufaika na hatua hiyo ya Serikali ni pamoja na vijiji vya Mbeya, Ishihimulwa, Gilimba, Nzubuka, Izugawima, Kingwanhoma, Usagali, Bukala pamoja na kijiji cha Uwimate

Kamati ya Mwaziri 8 Wizara za Kisekta ikiwa wilayani Uyui mkoani Tabora juzi baadhi ya wajumbe wake walilazimika kutumia usafiri wa pikipiki (Bodaboda) kufika sehemu ya maeneo ya vijiji ikiwemo kijiji cha Ishihimulwa ili kutoa mrejesho wa utekelezaji Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji.

Ikiwa katika kijiji cha Ishihimulwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta William Lukuvi ilibidi ahutubie wakazi wa eneo hilo akiwa kwenye helikopta baada ya wananchi kuamua kuufuata ujumbe wa Mawaziri hao eneo ilipotua badala ya sehemu iliyopangwa kwa mkutano wa hadhara.

Aidha, Kamati ya Mawaziri 8 pia ilifika kijiji cha Kangeme wilayani Urambo ambako huko Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwaeleza wakazi wa eneo hilo kuwa, mipaka ya hifadhi ya msitu wa Ulyankulu iheshimiwe na wananchi waendelee kusalia maeneo waliopo sasa.

‘’Pamoja na hifadhi ya Msitu kusajiliwa lakini mipaka yake iheshimiwe na wananchi mbaki maeneo yenu kama mlivyo na tutaicha timu ifanye tathmini hapa na tathmini hiyo itakuwa shirikishii’’ alisema Waziri Lukuvi.

Mawaziri waliokuwa kwenye msafara huo, kila mmoja alielezea mipango ya Serikali kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi kwenye vijiji 975.   Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki alisema, ni vyema wananchi wakaheshimu mipaka ya maeneo ya hifadhi na kuacha tabia ya kuvamia maeneo hayo kwa kuwa siyo ya kuchungia mifugo.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso aliwaeleza wananchi wa jimbo la Urambo kuwa, pamoja na Kamati ya Mawaziri kujikita kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi, Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha tatizo la maji kwenye jimbo la Urambo ambapo sasa jimbo hilo litapelekewa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria.

‘’Napenda niwape salamau kutoka kwa mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan emeelekeza baada ya kilio cha muda mrefu ule mradi wa maji wa ziwa Victoria unaopita Igunga na Nzega pamoja na Tabora sasa utaletwa pia kwenye jimbo la Urambo’’ alisema Aweso.

Manaibu Mawaziri nao waligusia mikakati ya Wizara zao kuhusu vijiji vilivyorasimishwa katika maeneo ya hifadhi. Mary Masanja Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii aliwahimiza wananchi kuhakikisha hawavamii tena hifadhi na waheshimu mipaka ya hifadhi kwa kuacha kufanya shughuli zinazoweza kuharibu misitu.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Chande aliwaambia wakazi wa vijiji hivyo kuwa, utunzaji mazingira siyo suala la hiari kwa kuwa wananchi wanatakiwa kuyatunza na wasipofanya hivyo mazingira hayo yataharibu mfumo wa maisha.

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde alisema, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan mbali na kupeleka fedha za maendeleo kwenye Tarafa na maeneo mbalimbali nchini haijalisahau jimbo la Urambo mkoani Tabora linaloongozwa na Magreth Sitta ambapo kwa upande wa barabara imetenga takriban bilioni 1.5 kwa ajili ya barabara za vijijini.

Mawaziri wa Wizara za Kisekta wamemaliza ziara kwenye mkoa wa Tabora ukiwa ni mkoa wa 4 tangu kuanza ziara yao ya kutembelea mikoa 10 na siku ya Ijumaa tarehe 15 Oktoba 2021 wanaendelea kwenye mkoa wa Mara kwa lengo la kupeleka mrejesho wa maamuzi ya baraza la mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (wa tano kushoto) akiwa kwenye picha na Mawaziri wa Kisekta pamoja na viongozi wa mkoa wa Tabora walioongozwa na mkuu wa mkoa huo Dkt Batilda Burian (Katikati) katika kijiji cha Kangeme wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta kutoa mrejesho wa utekelezaji maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa katika usafiri wa pikipiki (Bodaboda) katika kijiji cha Ishihimulwa wilayani Uyui mkoani Tabora wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta kutoa mrejesho wa utekelezaji maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta wakati ujumbe wa Mawaziri hao ukitoa mrejesho wa utekelezaji maamuzi ya Baraza la Mawaziri kwa mkoa wa Tabora juzi kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde akizungumza wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta kutoa mrejesho wa utekelezaji maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 mkoani Tabora juzi.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki (Kulia) akiwa na Manaibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja (wa pili kulia) na Hamad Chande Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta kutoa mrejesho wa utekelezaji maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 mkoani Tabora juzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...