Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Bw. Hery Mkunda akieleza jambo wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi PURA. 



KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Bw. Hery Mkunda na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula wameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwa kushirikisha watumishi wa Taasisi hiyo katika kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu. Viongozi hao wametoa pongezi hizo katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi PURA kilichofanyika tarehe 15 na 16 Oktoba, 2021 mkoani Morogoro kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/21 na utekelezaji wa majukumu kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/22.

Akitoa maoni katika kikao hicho, Bw. Hery ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi PURA ameeleza kuwa kushirikisha watumishi wa Taasisi katika kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ni jambo la msingi sana na litasaida kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. “Niipongeze PURA kwa kuandaa kikao hiki muhimu na nimatumaini yangu kuwa watumishi watajadili kwa kina na kufanya tathmini ya mwenendo wa utendaji kazi wa Taasisi, kufahamu maeneo ambayo Taasisi imefanya vizuri, maeneo yanayohitaji kutiliwa mkazo na kutoa ushauri wa nini kifanyike kuongeza ufanisi zaidi”, alieleza Bw. Hery.

Kwa upande wake Bi. Sara alieleza kuwa PURA imefanya jambo la kupigiwa mfano kwa kuwa sio Taasisi nyingi zenye utaratibu wa kuhusisha watumishi kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu waliyojipangia katika mwaka wa fedha husika. Aidha, Bi. Sara ameipongeza PURA kwa kutoa fursa kwa watumishi kupitia wawakilishi wao ambao ni wajumbe wa Baraza kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu waliyojipangia

Baraza la Wafanyakazi PURA linaundwa na wajumbe 34 waliopatikana kwa mujibu wa miongozo ya uundaji wa mabaraza ya wafanyakazi. Kati ya wajumbe hao, wapo wajumbe wanaoingia kwa nyadhifa zao (Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi, Wakuu wa Idara na Vitengo, na Wajumbe wa Halmashauri ya Tawi la TUGHE); wajumbe wa kuchaguliwa kutoka Idara/Kitengo vya Taasisi; Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi PURA ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Mha. Charles Sangweni akifungua kikao cha Tatu cha Baraza kilicholenga kujadili taarifa za utekelezaji wa Taasisi hiyo

Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula akichangia mada katika kikao cha Baraza. 

Mkurugenzi wa Masuala ya Ufundi PURA, Mha. Danstan Asanga akifafanua jambo kwa wajumbe katika kikao cha Baraza 

Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi PURA, Bi Hawa Mniga akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu kwa wajumbe wakati wa kikao cha Baraza. 

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi PURA wakifuatilia Taarifa zilizokuwa ziliwasilishwa katika kikao cha Baraza kilichofanyika mjini Morogoro 

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi PURA Mha. Charles Sangweni (mwenye miwani) na Katibu Msaidizi wa Baraza Bw. Ebeneza Mollel wakifuatilia kwa makini michango inayotolewa na Wajumbe wa Baraza.

Wajumbe wanaounda Baraza la Wafanyakazi PURA wakiwa katika picha ya pamoja.

 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...