Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

BAADA ya Biashara United Mara kushindwa kusafiri kuelekea nchini Libya kutokana na kile kilichoelezwa kukosekana kwa vibali vya anga vya Kimataifa nchini Sudan, Sudan Kusini na kibali cha kutua Benghazi, Libya ambapo mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Al Ahly Tripoli SC utachezwa hatma ya Klabu hiyo kutoka mkoani Mara, Tanzania inasubiriwa maamuzi ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Taarifa zinadai tayari Klabu ya Al Ahly Tripoli SC imefika kwenye uwanja wa mchezo huo na tayari imepewa ushindi wa mezani baada ya wapinzani (Biashara United) kushindwa kutokea kwenye dimba hilo kwa sababu hizo zilizoelezwa.

Maamuzi ya Al Ahly Tripoli kusonga mbele ya Michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inasubiriwa kutoka CAF baada ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kueleza kuwaandikia barau CAF kuomba kusogezwa mchezo huo hadi Oktoba 27, 2021 kutokana na Timu hiyo kukosa vibali vya anga vya Kimataifa.

Biashara United Mara walitarajiwa kucheza leo Jumamosi Oktoba 23, 2021 ikiwa ni mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Al Ahly Tripoli ambapo mchezo wa mkondo wa kwanza Biashara United waliibuka na ushindi wa bao 2-0 katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...