MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imemuhukumu Mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba kulipa fidia ya Sh. Bilioni sita kwa Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bernard Membe ikiwa ni fidia ya kumchafua kupitia vyombo vyake vya habari.

Hukumu hiyo imetolewa leo Oktoba 28,2021 na Jaji Joacquine De Mello ambaye amesema mbali na kulipa kiasi hicho cha fedha pia ametoa zuio la kudumu la kutomkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake huku pia akitakiwa kulipa gharama za kesi.

Katika kesi hiyo namba 220 ya mwaka 2018, Membe anamdai Musiba fidia ya jumla ya sh. Bilioni 10.3 kama fidia kwa kumkashfu, kupitia magazeti yake ya Tanzanite.

Akifafanua hukumu hiyo, Jaji De Mello amesema katika fedha hizo,  Sh.Bilioni 5 ni fidia ya hasara halisi na Sh. Bilioni 1 hasara ya jumla.

Musiba katika kesi hiyo alishtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...