Na Joseph Lyimo


MAKUNDI maaalum ya wachimbaji madini, wavuvi, wakulima wa mashamba makubwa, wafanyabiashara na wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wamepatiwa uhamasishaji na kushiriki chanjo dhidi ya Uviko-19.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Simanjiro Dkt Aristidy Raphael amesema kuwa Halmashauri hiyo imejipanga katika kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kila siku.

Dkt Raphael amesema makundi mbalimbali ya wananchi wa wilaya hiyo wamepatiwa elimu na chanjo ya Uviko-19 ili kuhakikisha wanajikinga na janga hilo.

"Kama halmashauri tunaendelea kuhamasisha kwenye vijiji na vitongoji ikiwemo maeneyo ya makazi, ili kuhakikisha wananchi wa makundi mbalimbali wanaelewa.

Amesema katika kutekeleza mpango wa jamii shirikishi na harakishi na uhamasishaji dhidi ya chanjo ya Uviko-19 wameweza kukutana na makundi hayo na wameweza kuwapatia elimu na kuwajibu maswali yaliyokuwa yakiwatatiza hapo awali.

Amesema wananchi wengi walikuwa na maswali juu ya taarifa potofu kuhusu chanjo hizo na ziliwafanya wasiweze kuchanja illa kwa elimu waliyowapatia wameelewa na wamehamasika kuchanja.

Amekiri kuwa awali mwitikio ulikua ni mdogo ila baada ya kutoa elimu kila mahali wananchi wameweza kujitokeza na kuchanja kwa wingi.

Amesema wilaya hiyo ilipatiwa dozi elfu 1,000 mwezi Agosti, na mwezi Septemba na Oktoba wakaongezewa dozi 2,000 hivyo kuwa dozi 3,000 ambazo zimetumiwa na wananchi hao.

Mchimbaji wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani, Ally Ramadhani amesema idara ya afya ya wilaya hiyo, wametoa elimu kubwa juu ya chanjo hivyo wachimbaji nao wakashiriki kuchanja.

"Awali tulipotoshwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya chanjo hii ila kutokana na elimu ya wataalamu wa afya wakatuelimisha na sasa tumechaja" amesema.

Mvuvi wa bwawa la Nyumba ya Mungu, Christopher Elias amesema wavuvi wa eneo hilo wamepatiwa chanjo hivyo kujikinga na janga hilo la Uviko-19.

Mkulima wa mashamba makubwa wa kijiji Cha Naberera, Onesmo Lesakwi amesema wamepatiwa chanjo ya Uviko-19 baada ya kupatiwa elimu hivyo wanaishuku serikali kwa hatua hiyo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...