NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

MBunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ameahidi kulivalia njuga suala la changamoto ya upatikanaji wa maji Safi na salama  inayowakabili wananchi wa kata ya Pangani hususan wakinamama.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa mtaa wa kidimu uliopo kata ya Pangani ikiwa ni ziara yake ya kikazi yenye lengo la kusikiliza kero na changamoto za wananchi ikiwemo kutembelea miradi ya maendeleo.

Koka ambaye katika ziara hiyo ameweza kukagua pamoja na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo mradi mkubwa wa maji wa kawe ambao ukikamilika utakuwa ni mkombozi mkubwa wa wananchi wa kata ya Pangani na maeneo mengine ya jirani.

Koka alisema kuwa licha ya kutembelea miradi huo wa maji lakini pia ameweza kutembelea miradi wa daraja ambalo pia amedai pindi litakapokamilika litawasaidia wananchi kuvuka kwa urahisi hasa katika kipindi Cha mvua.

"Nipo katika ziara yangu ya kikazi kwa wananchi wa kata ya Pangani lakini wakati naingia nimeweza kupokelewa na kundi la wakinamama wakiimba nyimbo za kuomba huduma ya maji kwa hivyo katika hili nitahakikisha ninalisimamia kwa hali na Mali,"alisema Koka.

Pia Koka alifafanua kuwa kwa Sasa katika kata ya Pangani Kuna miradi miwili ya maji ambayo inatekelezwa na mmoja ukiwa wa eneo la vikawe na unatarajiwa kumalizika mwakani na utakuwa ni msaada mkubwa.

Aidha MBunge aliuagiza uongozi wa Dawasa kuharakisha zaidi ukamilishaji wa mradi huo mkubwa ili kuweza kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kusaka huduma ya maji.

Katika hatua nyingine alibainisha kuwa ataendelea kuboresha sekta ya afya kwa kuweka mikakati kabambe ya kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo Cha afya lengo ikiwa ni kuwasogezea huduma karibu ya matibabu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Pangani Agustino Mdachi alimpongeza Mbunge huyo kwa kufanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi kwa lengo la kuzichukua na kuzitafutia ufumbuzi.

Nao baadhi wa wananchi wa mtaa wa kidimu kata ya Pangani akiwemo Ester Shija wameniomba Mbunge huyo kuwasaidia upatikanaji wa huduma ya maji Safi na salama kwani kwa Sasa wanateseka Sana sambamba na kuboresha huduma ya afya.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya Pangani hawapo pichani wakati wa ziara yake ya kikazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...