Na Khadija Kalili, 
KATIKA kupambana na maradhi ya ugonjwa Covid-19 Mkoa wa Pwani umepokea chanjo ya kupambana na ugonjwa huo dozi 25,000 baada ya dozi za awali 30,000 kumalizika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Kibaha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Gunini Kamba alisema kuwa baada ya dozi za awamu ya kwanza kumalizika  tayari dozi za awamu ya pili zimshaingia.

Dkt. Kamba alisema kuwa dozi hizo kimkoa zitaanza kutolewa watu wataendelea kupatiwa huduma hiyo kwa dozi mpya aina ya Sinopharm ambayo mtu atachanjwa mara mbili tofauti na ilivyokuwa chanjo ya JJ ambayo ilikuwa mtu anachanjwa mara moja tu.

“Mara baada ya serikali kupokea chanjo wahudumu wanaochanja chanjo hiyo walipata mafunzo ya namna ya kuchanja ambapo tayari wameshamaliza mafunzo hayo na sasa wanaendelea na kazi ya kuhudumia wananchi,”alisema Dkt. Kamba. 

Alisema baada ya kupata awamu ya kwanza ya chanjo dozi 30,000 ilipokwisha waliomba dozi 1,200 ambazo nazo ziliisha ambapo Mkoa ulijipanga kusubiri dozi hii ya awamu ya pili kutoka nchini  China. 

“Chanjo hii dozi yake ni mbili hivyo mtu akichanjwa mara ya kwanza anakaa na baada ya siku 28 anachanja dozi ya pili hivyo anakuwa amekamisha chanjo yake,”alisema  Dkt. Kamba.

Aidha alisema kuwa zoezi hilo kwa awamu ya kwanza lilienda vizuri licha ya mwanzo watu kuwa na dhana tofauti na kufanya kuwe na ugumu lakini baada ya kupatia elimu wakaazi wa Mkoa wa Pwani  walijitokeza kwa wingi na kuchanja bila ya wasiwasi wowote. 

“Tunatoa wito kwa wale ambao hawakubahatika kuchanja chanjo ya awamu ya kwanza wajitokeza kwenye awamu hii ya chanjo ya sasa ili kupambana na ugonjwa wa Covid 19 ambapo chanjo hiyo ni salama na haina shida yoyote,”alisema Dkt. Kamba.

Alisema kuwa chanjo hiyo itatolewa kwenye maeneo yale yale ambapo ilipokuwa inatolea chanjo ya awali kwenye vituo vya Afya na Zahanati na sehemu zinazotoa chanjo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...