Na Mwandishi wetu,Michuzi TV - Rufiji

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, John Kayombo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia halmashauri hiyo Sh bilioni 1.350.

Fedha hizo ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mipya ya mpango wa maendeleo ya ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Uviko-19).

Akitoa mchanganuo wa fedha hizo na miradi iliyoainishwa, Kayombo  amesema Sh milioni 720 zitatumika katika ujenzi wa madarasa 36 ya shule za sekondari na Sh milioni 240 kwa ujenzi wa madarasa 12 ya shule shikizi katika halmashauri hiyo.

"Pamoja na hayo pia fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa jengo la dharura ambazo ni Sh milioni 300 na Sh milioni 90 tutazitumia kwenye ujenzi wa nyumba katika cha kutolea huduma za afya katika halmashauri yetu.

"Kwa mchanganuo huo tunapata jumla ya fedha zote tulizopewa na Rais Samia kuwa Sh bilioni 1.350, tunamshukuru sana na tunatarajia kuzitumia fedha hizo katika miradi iliyokusudiwa," amesema Kayombo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...