* Wazazi, walezi na jamii yashauriwa kushiriki sensa ya watu na makazi kwa kutoa takwimu sahihi za watoto wenye changamoto ya ulemavu.


SHIRIKA linaloshughulika na masuala ya watoto wenye ulemavu 'Najim Foundation' (NACHO,) limepongezwa kwa jitihada za kuwasaidia watoto wenye ulemavu jambo linalounga mkono juhudi na azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza jamii, mashirika yasiyo ya Serikali na kimataifa kushiriki katika kusaidia watu wenye ulemavu hasa katika mahitaji ya msingi ikiwemo vifaa mwendo na elimu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa shirika hilo hafla iliyoenda sambamba na ugawaji wa vifaa mwendo wa watoto 40 wenye ulemavu, Mkurugenzi wa Ushirika wa Wanawake Wajasiriamali (GCI,) Fatma Kange amesema shirika hilo limekuwa ya mfano na mwavuli utakaowasaidia wanawake wanaotunza watoto wenye ulemavu kusema changamoto na uhitaji wao ambapo kila mmoja katika jamii, Serikali, Asasi za kiraia na mashirika ya Kimataifa ana wajibu wa kuonesha ushiriki kwa kuhakikisha watoto hao wanapata mahitaji ya kimsingi.

''Safari ya wanawake huwezi kuitafuta, kuna mapito mengi na changamoto nyingi zilizojificha, NACHO imeanzisha mwavuli imara na salama wa kusema changamoto zetu kama walezi wa watoto wetu wenye mahitaji mengi.... tuwatumie NACHO kueleza changamoto zetu na kuangalia namna ya kuzitatua pamoja kwa kushirikiana na Serikali na asasi za kiraia na kimataifa na kuwawezesha walezi wao wa karibu juu ya namna ya kujikwamua kiuchumi na sio kuwatumia watoto kama nyenzo ya kupata kipato.'' Amesema.

Amesema Serikali ya awamu tano imejibainisha wazi juu ya azma ya kutetea watu wenye ulemavu na wanawake kwa ujumla na kuitaka jamii  kutowaficha watoto hao hasa katika kipindi hiki ambapo Taifa linaelekea katika sensa ya watu na makazi.

''Mwaka ujao kutakuwa na zoezi la sensa ya watu na makazi, wazazi, walezi na jamii kwa ujumla tutumie fursa hii kutoa takwimu sahihi tuwatoe watu wenye mahitaji muhimu ili Serikali iweze kuwasaidia mahitaji ya msingi.'' Ameeleza.

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirika hilo Jane Wasira amesema, mwanzilishi wa shirika hilo Kibibi Bayaka aliona changamoto wanazopitia wanawake wanaolea watoto wenye ulemavu kupitia kijana wake mwenye ulemavu Najim (26,) na kuanzisha shirika hilo ili kuweza kuwakutanisha wanawake hao, kujadili changamoto zinazowakabili na kutafuta namna ya kuzitatua.

'' Shirika la Najim itatoa huduma za day care kwa watoto wenye ulemavu kuanzia wachanga hadi miaka 16 ambapo watakutana na kutojihisi wapo peke yao na wakiwa hapo kutakuwa na walimu watakaowafundisha masuala mbalimbali na madaktari wa mazoezi licha ya hayo vifaa mwendo, vifaa vya choo, vifaa vya kusimamia na vifaa vyaa mazoezi vitatolewa kwa watoto wanaotoka katika hali duni.'' Amesema.

Vilevile amesema pia kwa wanawake waliotelekezwa na watoto hao kuna mpango wa kutoa ruzuku na mafunzo ya ujasiriamali ili waweze kushiriki shughuli za kijamii na kiuchumi ili kukomesha shughuli za kuomba barabarani jambo ambalo huwaathiri watoto hao kisaikolojia.'' Amesema.

Awali Mwanzilishi wa shirika hilo Kibibi Bayaka aliwataka wanawake na walezi wa watoto hao kutokata tamaa na kutowatumia watoto hao katika shughuli za kuomba barabarani na kuahidi kushiriki katika kutatua changamoto zinazowakabili na kuwashauri kuutumia vyema mwaka ujao katika sensa ya watu na makazi kwa kutoa takwimu sahihi ili waweze kupata mahitaji muhimu kutoka kwa Serikali inayoongozwa na Rais mwanamke na mpigania haki za wanawake na walemavu Samia Suluhu Hassani.


Mwenyekiti wa Najim Foundation (NACHO,) Jane Wasira (kushoto) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa shirika hilo na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana na wanawake wanaolea watoto wenye changamoto ya ulemavu, Leo jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa Shirika hiloKibibi Bayaka ambaye pia analea mtoto mwenye changamoto ya ulemavu akizungumza katika warsha hiyo na kuwataka akina Mama hao kutokata tamaa katika kuwalea watoto hao.


Mkurugenzi wa Ushirika wa Wanawake Wajasiriamali (GCI,) Fatma Kange akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vifaa mwendo 40 vilivyotolewa kwa watoto wenye uhitaji.








Matukio mbalimbali katika warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Ushirika wa Wanawake Wajasiriamali (GCI,) Fatma Kange akizungumza katika warsha hiyo ambapo ameipongeza NACHO kwa kuwakutanisha wanawake wanaolea watoto wenye nchangamoto yenye ulemavu na kuwataka kushiriki sensa ya mwaka ujao kwa kutoa takwimu sahihi ili Serikali iendelee kuwasaidia mahitajiya msingi kwa watoto hao.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...