Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KOCHA Etienne Ndayiragije amefutwa kazi ya kuifundisha timu ya Klabu ya Geita Gold FC, baada ya kuwa na matokeo yasiridhisha katika michezo yake minne ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu huu wa 2021-2022, ulioanza kutimua vumbi mwishoni mwa Septemba, 2021

Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo imeeleza pande zote mbili zimefika makubaliano ya kusitisha mkataba huo kuanzia Oktoba 23, 2021, kutokana na Kocha huyo kushindwa kufika malengo waliyokubalina na Klabu.

Imeeleza pia timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Msaidizi Fredy Felix Minziro hadi taratibu na mchakato wa kumpata Kocha Mkuu utakapo kamilika. Klabu hiyo imemshukuru Kocha Ndayiragije katika kipindi chote alichokuwa Klabuni hapo.

Ndayiragije aliingia mkataba wa miaka miwili na Klabu hiyo na tayari amefutwa kazi akiwa na michezo minne ya Ligi hiyo. Mchezo wa kwanza alicheza dhidi ya Namungo FC mkoani Lindi na alipoteza kwa bao 2-0, mchezo wa dhidi ya Yanga SC alifungwa bao 1-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na alicheza nyumbani Uwanja wa Nyankumbu, Geita alipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, sare nyingine ya 1-1 dhidi ya Mbeya City FC hapo hapo Nyankumbu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...