Na Prof Mark Mwandosya

PICHA ya kihistoria ya Mwalimu Nyerere iliyo hapo chini imesambaa sana, hasa kwenye mitandao ya kijamii, na zaidi tarehe 14 Oktoba,  siku ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa (Siku ya Nyerere, Nyerere Day). 

Wengi mmeniuliza ni nani hao? wapi hapo? na ilikuwa lini?

Kwa kumbukumbu ilikuwa tarehe 4 Agosti mwaka 1993, nilipomtembelea Mwalimu nyumbani kwake Butiama, wakati huo nikiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Walio katika picha, kuanzia kulia ni: Ndugu Nzungu, aliyekuwa Afisa Biashara Mkoa; Ndugu Joseph Nyerere (Mdogo wa Mwalimu, marehemu); Ndugu Mgaya, aliyekuwa Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Nguo cha Musoma (MUTEX); Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; Mhandisi Mageni (Marehemu); wengine wawili ambao siwakumbuki; na mimi (Mark Mwandosya) kushoto kabisa tukiongea na Mwalimu.

Mwenyezi Mungu amrehemu Mwalimu Nyerere na wengine wote waliotutangulia mbele ya haki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...