Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 31 Oktoba, 2021 amewasili Glasgow, Scotland kuhudhuria mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP26).

Mkutano huo unaoshirikisha Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Viongozi wa Kidini, Viongozi wa Taasisi za Biashara, Asasi za Kiraia na watu mashuhuri utafunguliwa rasmi tarehe 1 Oktoba, 2021 na kupokea hotuba za viongozi wa Mataifa mbalimbali kuhusu mikakati ya nchi zao katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, Mkutano huo wa COP26 unakusudia kujadili na kutoa maamuzi ya kuharakisha utekelezaji wa maazimio yaliyopo katika Azimio la Paris katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mhe. Rais Samia anatarajiwa kuhutubia mkutano huo tarehe 2 Novemba, 2021, ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajia kuueleza ulimwengu kupitia hotuba hiyo hatua ambazo Tanzania imepiga katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi, changamoto inazokabiliana nazo katika mapambano hayo na pia masuala yanayotakiwa kufanyika ili kupiga hatua katika kufanikiwa kufikia malengo yaliyowekwa.

Mkutano huo umeandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza ambao ndio nchi mwenyeji na Rais wa Mkutano huo.


Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...