Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani akikagua banda maalumu la mapishi ya vyakula vya asili alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali kabla ya hajazindua jana maadhimisho ya wiki lishe Kitaifa Mkoani humo.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani akiwahutubia wakazi wa Tabora na wageni kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini ambao walishiriki uzinduzi jana wa maadhimisho ya wiki lishe Kitaifa Mkoani humo

Picha na Tiganya Vincent

*****************************

NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani ameagiza kila shule ihakikishe imepanda miti ya matunda katika maeneo yao.

Hatua hiyo inalenga kuongeza wingi wa matumizi ya matunda kwa ajili ya wanafunzi wawapo shuleni na kukamilisha mzunguko wa lishe bora.

Balozi Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya lishe ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Tabora chini ya kauli mbiu Lishe bora ni kinga thabiti ya magonjwa kula mlo kamili fanya mazoezi kwa bidii kazi iendelee.

Balozi Dkt. Batilda alisema hata kauli mbiu ya mwaka huu inasisitiza ulaji wa mlo kamili hauwezi kukamilika bila kuwepo kwa tunda katika chakula.

Aliwataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote Mkoani kuhakikisha wanawahimiza wananchi wakiwemo wanafunzi kupanda miti ya matunda ya aina mbalimbali katika maeneo yao.

Balozi Dkt. Batilda alisema hatua hiyo itaongeza upatikanaji wa matunda kwa ajili ya wao kula na yale ya ziada watauza na kujiatia fedha kwa ajili shughuli zao za maendeleo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Watendaji katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI Tumbi) kuhakikisha inasambaza teknolojia ya upandaji wa miti ya matunda na ile ya dawa asili ili isitoweke.

Alisema baadhi ya matunda pori yanafaida nyingi mwili ikiwemo kutumika kama tiba na kinga mwilini.

Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Batilda aliwataka wakazi wa Tabora na wageni waliopo katika maadhimisho hayo kutembelea eneo maalumu la mapishi ya vyakula vya asili kwa ajili ya kujifunza mapishi mbalimbali.

Alisema vyakula hivyo ni muhimu kwa kulinda afya kwa kuwa vinatumia viungo vya asili kama vile karanga na havitumii mafuta mengi.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kilele cha maadhimisho ya wiki ya lishe kitafanyika Jumamosi ya wiki hii ambao Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda alisema kwa kuwa Mwezi ujao wanaanza zoezi la kutoa chakula mashuleni atakwenda usimamia zoezi la upandaji wa matunda ili wanafunzi wanaokula chakula mchana wapate na matunda kwa ajili ya kukamilisha mlo kamili.

Wakati huo huo Wakuu wa Wilaya wamesaini Mkataba wa utekelezaji wa masuala ya lishe na Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili waweze kusimamia vizuri masuala ya lishe.

Akizungumza baada ya kuwasainisha mikataba hiyo , Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda aliwataka kuhakikisha masuala ya kuhamasisha lishe ni ajenda ya kudumu.

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitambua umuhimu lishe na ndio maana akasisi na kusisitiza masuala ya lishe hapa nchini wakati akiwa Makamu wa Rais.

Balozi Dkt. Batilda alisema Rais Samia alitambua kuwa kupitia lishe bora Watoto wanaozaliwa wanakuwa na king ana afya bora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...