Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )Taifa, Samia Suluhu Hassan ameielekeza UWT kufanya tathmini na kuandaa taarifa ya namna mwanamke alivyokombolewa kifikra,siasa ,kiuchumi pamoja na kuwaasa watafiti na waandishi wa sayansi ya historia kuandika historia ya muasisi na  shujaa wa kike wa kupigania Uhuru  katika harakati za ukombozi wa Tanganyika ,Bibi Titi Muhammad kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

Ameutaka pia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT ) kusimamia changamoto ya unyanyasaji wa kijinsia na baadhi ya wanawake kuacha kuwa sehemu ya kuchochea unyanyasaji huo ikiwemo wa watoto .

Pamoja na hayo ,Samia amekemea vitendo vya kuanza Kampeni za chinichini wakati tukielekea katika uchaguzi wa ndani ya Chama 2022 na amewaasa wanawake kujitokeza kugombea wakati ukifika .

Akihutubia mkutano wa kuadhimisha Kilele Cha wiki ya UWT kitaifa ,na kumuenzi mwanamama mpigania  Uhuru ,shujaa ,shupavu na muasisi Bibi Titi Muhammad aliyezaliwa Rufijii Mkoani  Pwani ,pia aliuagiza Umoja huo wakati ukielekea katika mkutano wao mkuu waandae taarifa ya namna walivyomkomboa mwanamke kifikra,kisiasa na kiuchumi toka mwaka 1961 .

Samia aliwasihi wanawake wafuate mfano wa kuigwa wa muasisi Bibi titi Muhammad na harakati zake za kushiriki kudai Uhuru.

Aliwapongeza UWT kuadhimisha siku hiyo Rufiji kwa kumuenzi muasisi Bibi Titi na kuwasihi kukataa kutumika kwa maslahi ya wengine .

"UWT  wameamua kumuenzi mwanamke huyu wa shoka ,ambae alishirikiana na baba wa Taifa Mwl. Nyerere na Rajabu Diwani kupigania Uhuru na kuhamasisha wanawake wajiunge na TANU.;'"

"Katika harakati za kumuenzi kifikra kiuchumi bado Kuna Safari ndefu ya kumfikia mwanamke kifikra ,kiuchumi na kisiasa."alifafanua Samia.

Samia alisema UWT inapaswa kuja hali ya tathmini ya namna mwanamke wa Tanzania kutoka Safari ya Bibi Titi hadi Rais Samia mwanamke amekombolewa kwa namna gani toka 1961 kumkomboa mwanamke kiuchumi kisiasa na kifikra .

Alisema wakati UWT  ikiasisiwa ilikuwa ni kuwaunganisha wanawake na kumkomboa mwanamke hivyo Ni wakati wa kujitafakari kupitia hayo na kuja na tathmini ili endapo kuna changamoto zifanyiwe kazi .

Aliipongeza UWT kuongeza nguvu kwa chama cha Mapinduzi na kwa hakika imefanya mambo makubwa ikiwemo kuanza ujenzi wa ofisi ya makao makuu pale Dodoma na kuanzisha miradi mbalimbali kujiinua kiuchumi .

Akielezea fedha zilizoelekezwa Mkoani Pwani ,,Samia alifafanua imepatiwa bilioni  13.39 ikiwa bilioni 2.2 zimeelekezwa katika madarasa 429 shule za sekondari na vyumba 108 kwenye shule shikizi na afya Kibaha ,Kisarawe .

Milioni 30.8 ujenzi wa barabara kutoka asilimia 9 hadi asilimia 41 ujenzi wa barabara kuhakikisha kuwa na mtandao wa barabara hawataki kuona barabara za vumbi .

Ameahidi kutekeleza barabara zote  zilizopo katika utekelezaji wa ilani Mkoani hapo.

Samia alieleza , upande wa barabara Wakala wa Barabara Vijijini TARURA imeongezewa bilioni 43 kutoka bilioni 9 na sh.bilioni 41 imeshatolewa kutekeleza usambazaji wa umeme katika vijiji 447 na kati ya hivyo vijiji 89 bado ambapo wakandarasi wapo site .

Akizungumza tatizo la umeme mdogo licha ya mkoa kuwa ukanda wa viwanda suala hili linashughulikiwa .

Nae Mwenyekiti wa UWT Taifa ,Gaudensia Kabaka amesema ,katika maadhimisho hayo wametembelea watoto yatima Ikwiriri,wagonjwa hospital ya wilaya ya Rufiji ambapo wametoa mashuka 100 na  kutoa taulo 2,500 kwa wanafunzi wa kike shule ya sekondari ya wasichana Ikwiriri na Utete.

"Tumeamua kuadhimisha kilele hicho Rufiji kwa sababu ya historia ya mama na mwanamke shupavu aliyemsaidia Baba wa Taifa Mwl.Nyerere kupigania Uhuru ambayo kwasasa tunaelekea kutimiza miaka 60 ya Uhuru,"

"Wiki ya UWT ilivyoanza ilianzishwa na chama Cha TANU ilikuwa sehemu ya wanawake wa TANU na Mwl.Nyerere alikuwa akisaidiwa na Bibi Titi, ambae alikuwa mhamasishaji mzuri ,muasisi na alikuwa Shupavu "

Akielezea wiki hiyo,Kabaka alisema siku ya leo inakwenda kumgusa kila mwanamke kwa kuleta mabadiliko chanja  ya kiuchumi ,ambapo kauli mbiu Ni "TUNAHUSISHA KUMKOMBOA MWANAMKE KIUCHUMI ,KIFIKRA NA KISIASA.

Kabaka alimpongeza Rais Samia kwa kulitangaza Taifa kiutalii na kuwa mlinzi wa Kwanza wa raslimali za nchi na kuhakikisha uchumi wa nchi unakua.

Katibu wa UWT Taifa Philis Nyimbi ameeleza wanaendelea kumuunga mkono kwa kutekeleza miradi mikubwa na kuitendea haki ilani ya CCM.

Alimshukuru kwa kumtetea mnyonge ,na wao wameendelea kuanzisha Miradi ya kiuchumi na sasa wanatarajia kuachana na kutegemea kutumia ofisi zilizopo ndai ya ofisi za chama ambapo wameanza ujenzi wa ofisi itakayogharimu milioni 378 .

Philis alieleza wataendelea kuthamini kazi anazofanya Rais Samia na namna anavyoendelea kupambana na Uviko 19 

Alieleza kuwa fedha trilioni 1.3 zilizotolewa kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo italeta tija sambamba na bilioni 1.4 kwaajili ya ujenzi wa madarasa na vituo vya afya.

Nae Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge akitoa salamu za Serikali alieleza, ni dhahiri Rais  Samia anapita katika nyayo za Bibi Titi kwa kuwa Shupavu .

Miradi ya maji iliyopatiwa fedha kupitia DAWASA bilioni 222,RUWASA bilioni 21 , TARURA imeongezewa bilioni 43 kutoka bilioni 9, pia mradi mkubwa wa bwawa la umeme Stigo-Rufiji tilioni 2.8 zimeshalipwa ,mradi wa Daraja jipya WAMI bilioni 72,Mradi wa reli ya kisasa (SGR) ambapo pia mkoa kwasasa una jumla ya viwanda 1,438 hali inayowezesha kuinua sekta ya uwekezaji kimkoa.

Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Muhammed Mchengerwa alisema jukumu letu ni kuendeleza fikra na hekima za Bibi Titi Muhammad na Ni muasisi aliyesanifu na kudhibiti minyororo ya unyanyasaji wa kijinsia .

Alisema wanaRufiji wanapongeza juhudi za Rais Samia na kuendeleza nyayo za Bibi Titi kwa kuweka usawa na haki .

"Kwa hakika umethibitisha hili kwa vitendo kwa kuwaongezea watumishi kuwapandisha madaraja na kuweka usawa wa kimaamuzi kwa kuteua wanawake wengi katika nafasi mbalimbali za uongozi".

Mchengerwa alizungumzia  changamoto ya tatizo la wafugaji kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima ,ameomba aridhie mifugo sasa ipelekwe Kisarawe -Mkuranga ili kupunguza kero hiyo.

Hata hivyo aliongeza changamoto nyingine ni
Kupita Dar es salaam wanapokwenda mikoani wameomba Rais ardhie kuanza mchakato wa kupata mkoa mpya ili kusogeza huduma.

Naibu Katibu Mkuu Bara  (CCM) Christina Mndeme alisema Samia anaupiga mwingi,Ni Rais mpole ,anapeleka maendeleo mbele ,Samia ni mchapakazi na asiye mbaguzi.

Alisema ukimkwamua mwanamke umekomboa Taifa hivyo wanawake wajitambue kwakuwa wanawake ni jeshi kubwa, lazima watangaze mambo makubwa yanayofanywa na Serikali na Rais Samia.

Aliomba wanawake , Samia asiwatoke midomoni mwao kwa sala na maombi ili apate nguvu ya kulisimamia Taifa na kwa hakika Tanzania inakwenda kubadilika.

"Shughuli hii ni utekelezaji wa ilani  ,CCM inaendelea kutoa maelekezo kwa kamati za mkoa kusimamia  asilimia 10 ya mikopo isiyo na riba kwa makundi ya vijana wanawake na walemavu na kuhakikisha zinatumika ipasavyo .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...