Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya elimu nchini imetumia shilingi Bilioni 46.476 kwa ajili ya kuchapa vitabu nakala 20,943,989 vya elimu kuanzia ngazi ya Awali,Msingi,Kundirika,Maandishi yaliyokuzwa pamoja na Sekondari.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 15/ 20021 na Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia ,Mhe.Profesa Joyce Ndalichako katika uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vitabu hivyo katika halmashauri zote 184 nchini kwa uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi wawili.

"Wizara itaendelea kusimamia kila pesa inayoletwa na Serikali katika kuendeleza Elimu nchini hivyo napenda kutoa shukrani zangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mhe.Samia Suluhu kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya elimu"alisema Mhe.Ndalichako.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt Aneth Komba amesema kuwa vitabu hivyo vimeandaliwa na wataalamu wa TET kwa kushirikiana na wataalamu wengine kutoka vyuo vikuu, vyuo vya Ualimu pamoja na walimu kutoka shule za Sekondari na Msingi.

Zoezi la usambazaji wa vitabu hivyo limeanza leo mara tu baada ya uzinduzi.

Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce Ndalichako akikata utepe kuashiria kuanza kwa uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vitabu vya Kiada Shule za Msingi na Sekondari vilivyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania,vitabu hivyo vitasambazwa katika halmashauri zote 184 nchini
Mkuu wa kikosi 95 kikosi cha usafirishaji JWTZ,Kanali Benjamini Kisinda akifafanua zaidi mbele ya Waandishi wa habari namna watakavyosambaza vitabu hivyo nchi nzima

Baadhi ya Magari ya JWTZ yatakayotumika kusambaza vitabu hivyo nchi nzima

Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce Ndalichako sambamba na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo wakiwasili kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa vitabu vya Kiada Shule za Msingi na Sekondari vilivyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania,vitabu hivyo vitasambazwa katika halmashauri zote 184 nchini.Pichani kulia ni Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Elimu Gerald Geofrey Mweli



Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce Ndalichako akiwapungia mkono Wageni waalikwa mbalimbali wakati akielekea kukagua ghala la vitabu,ambapo zoezi la uzinduzi wa usambazaji wa vitabu hivyo vya Kiada Shule za Msingi na Sekondari vilivyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania umeanza leo .

Pichani kati ni Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce akieleza jambo kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba wakati akiendelea kukagua vitabu vilivyomo ndani ya ghala hilo,kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akishuhudia




Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce akimuonesha jambo kwenye moja ya kitabu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo,pichani kulia ni Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba akishuhudia

Pichani kati ni Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce akieleza jambo kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba wakati akiendelea kukagua vitabu vilivyomo ndani ya ghala hilo,kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo na pichani kati ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya Elimu Gerald Geofrey Mweli

Sehemu ya vitabu ambavyo vinatarajiwa kusambazwa katika halmashauri zote 184 nchini


Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu nchini Dkt.Aneth Komba akimueleza jambo Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce
Mgeni rasmi Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Profesa Joyce sambamba na Wageni wa Meza Kuu wakitoka ndani ya ghala mara baada ya kushuhudia shehena ya vitabu vya Shule ya Msingin na Sekondari vinavyotarajiwa kuanza kusambazwa leo nchi nzima

Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia tukio hilo


















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...