Waandishi wa habari pamoja na wataalamu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi inayofanyika agamoyo Mkoani Pwani.
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Bagamoyo

SHIRIKA lisilo la kiserikali la HakiMadini limewakutanisha waandishi wa vyombo vya habari nchini katika semina maalum ya.siku tano kwa lengo la kuwajengea uwezo pindi wanapotaka kuandika au kutangaza habari zinazohusu nishati jadidifu.

Kama inavyofahamika wanahabari ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi hasa ikizingatiwa kwa kiasi kikubwa ndio wanaoandika na kusambaza habari zinazohusu maendeleo ya nchi.

HakiMadini ipo katika kuhakikisha taarifa nyingi na sahihu zinafika maeneo mengi ya nchi na kila Mtanzania atambue umuhimu wake katika maendeleo ya nchi.

Maofisa wa HakiMadini na wataalam wa masuala ya nishati jadidifu wameeleza kuwa matumaini yao baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo waandishi wa habari waliopata nafasi ya kushiriki watakuwa wamepata uelewa kuhusu nishati jadidifu,hivyo hata watakapokuwa wakitoa taarifa watakuwa wanafahamu mambo mengi.

Semina hiyo iliyoandaliwa na HakiMadini imeingia siku ya pili kwa watalaamu kutoka taasisi za umma na binafsi wamekuwa wakitoa mada kwa lengo la kuhakikisha waandishi waliopo wanaondoka na kitu kichwani ambacho kitakuwa mwanga utakaomuongoza katika kuandika au kutangaza habari zinazohusu nishati jadidifu.

Kwa upande waandishi wa habari akiwemo Mwandishi wa Gazeti la Jamvi la Habari Hafidhi Kido amezungumzia umuhimu wa semina hiyo kwa waandishi wa habari huku akifafanua.

"Semina au warsha namna hii zimechelewa kuja kwa sababu masuala ya nishati yana mabadiliko nakubwa duniani. Wananchi wanahitaji kuwa na uelewa juu ya rasilimali tulizonazo na namna ya kunufaika nazo.

"Ieleweke unapompa taarifa sahihi mwanahabari ni sawa na kuipa jamii nzima taarifa hizo. Lazima tujivunie kilicho chetu. Utajiri tulionao katika maji, eneo kubwa la ardhi pamoja na jua mwaka mzima ni faida kubwa kwetu."
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mada mbalimbali wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi inayofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.

Mjiolojia John Bosco,akitoa mada mbalimbali wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi iliyoanza inayofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.

Mkufunzi kutoka HakiMadini,akitoa mada wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi inayofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.


Baadhi ya washiriki katika semina hiyo iliyoandaliwa n Shirika la HakiMadini wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea.

Mtalamu wa masuala ya Nishati Mhandisi Arthur Karomba,akilezea mada mbalimbali kuhusu umeme jua wakati wa warsha ya kuwajengea uelewa wa sekta ya Nishati Jadidifu na Maendeleo ya Jamii waandishi wa habari iliyoandaliwa na HakiMadini kwa kushirikiana na wataalamu wa sheria kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na Wizara ya Nishati kuhusu utafiti wa fursa na changamoto za nishati jadidifu na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi inayofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakitoa maoni yao kuhusu nishati jadidifu na wengine wakisikiliza kwa umakini mkubwa wakati wa semina ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Shirika la HakiMadini.

Sehemu ya waandishi wakiendelea kujadiliana wakati wakiandika habari zinazohusu nishati jadidifu baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mmoja wa watoa mada kwenye semina hiyo.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...