Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KLABU ya Simba rasmi imetangaza kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu, Didier Gomes Da Rosa baada ya kuridhia ombi lake kuanzia leo Oktoba 26, 2021. Simba SC imeachana na Gomes Da Rosa sambamba na baadhi ya watu wake katika Benchi la Ufundi, akiwemo Kocha wa Makipa, Milton Nienov na Kocha wa Viungo, Adel Zrane.

Taarifa iliyotolewa na Menejimenti ya Klabu hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo ya kuachana na Kocha Mkuu imekuja baada ya majadiliano ya kina ya pande zote kuafikiana kwa mujibu wa mkataba na manufaa kwa wote.

Pia imeeleza kuwa Kocha Msaidizi Thierry Hitimana atakuwa Kocha Mkuu katika kipindi cha mpito akisaidiwa na Kocha Msaidizi Suleiman Matola.

Klabu hiyo imewashukuru Kocha Gomes na wenzake katika kipindi chote cha mafanikio walichotumikia Simba SC pamoja na kuwatakia kheri waendako.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...