Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) (wa saba kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester (kushoto kwa Balozi Mulamula) na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa tano kutoka kulia) pamoja na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku moja


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb).


Maongezi baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester yakiendelea. Maongezi hayo pia yamehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine, Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo, Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe. Nabil Hajlaouvi pamoja na viongozi mbalimbali.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine, (kulia) akiwa na Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo, pamoja na Mkurugezi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Swahiba Mndeme wakifuatilia kikao cha Waziri Mulamula na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester akieleza jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester leo Jijini Dar es Salaam


Mawaziri wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi leo Jijini Dar es Salaam








Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester leo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku moja
*******************************

Na Mwandishi Wetu, Dar

Tanzania na Ufaransa zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo ya kimkakati ikiwemo Nishati, Elimu, Kilimo na Miundombinu ambapo Ufaransa umekubali kukarabati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘Terminal Two’ Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester leo alipowasili Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Kumekuwa na Miradi ambayo Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lao la Maendeleo wamekuwa wakifadhili Miradi mbalimbali katika Sekta mbalimbali hapa nchini zikiwemo sekta za Nishati, Elimu, Kilimo na Miundombinu.

Mtakumbuka kuwa Ufaransa ndiyo waliojenga Uwanja wa Ndege wa “Termirnal Two” wa Julius Kambarage Nyerere sasa wanakuja na mradi wa kukarabati uwanja huo na kuufanya kuwa wa kisasa zaidi. Sasa hivi tu terminal three lakini terminal two imekuwa ikitumika na ndege zinazofanya safari zake za ndani hapa nchini,mradi huu ni moja kati ya mradi mkubwa na utakamilika hivi karibuni.

Waziri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Ufaransa, Mhe. Franck Riester yupo nchini Tanzania kuzindua safari za Shirika la ndege la Ufaransa ‘Fance Airline’ kutoka Paris hadi Zanzibar ambapo mara ya mwisho kwa shirika hilo kufanya safari zake hapa nchini ilikuwa mwaka 1974.

Septemba 15, 2021 Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Nabil Hajlaouvi alisema Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la ndege ‘Fance Airline’ inategemea kuanzisha safari mpya ya ndege kutoka Ufaransa moja kwa moja hadi Zanzibar kuanzia 19 Oktoba 2021.

Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Colin Powell.

“Kwa kweli Serikali ya Tanzania tumeshtushwa sana na kifo chake katika kipindi chake aliendeleza uhusiano wa Marekani na Mataifa mbalimbali, kwa kweli ni masikitiko makubwa tutamkumbuka daima,” Amesema Balozi Mulamula

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...