Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Vivutio vya Kiuchumi wa Ufaransa Franck Reister (watatu kushoto,) akiwa ameambatana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa duka la bidhaa za Ufaransa na Tanzania chapa " Aelia Duty Free" lililopo Terminal III katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.



WAZIRI  Wa Mambo ya Nje, Biashara na Vivutio vya Kiuchumi wa Ufaransa Franck Reister amesema uhusiano wa Tanzania na Ufaransa ni wa kudumu na kupitia duka jipya la kampuni ya Ufaransa ya chapa 'Aelia Duty Free Brand' lililopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Terminal III ni sehemu sahihi ya kubadilishana bidhaa za utalii na kukuza sekta hiyo.

Akizungumza jana wakati wa kuzindua duka maalumu la bidhaa mbalimbali ikiwemo vyakula, bidhaa za kimataifa na bidhaa za utalii Reister alisema, duka hilo ni alama ya umoja, amani na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na kupitia bidhaa zinapatikana hapo Tanzania itegemee watalii wengi kutoka Ufaransa na kuwahimiza watanzania kuendelea kudumisha umoja na uhusiano imara wa mataifa hayo.

" Duka hili ni la biashara za kimataifa na limetoa fursa kwa bidhaa za Tanzania kunufaika zaidi katika soko la kimataifa...niwahakikisshie kuwa Tanzania itapata watalii wengi kutoka Ufaransa na Ulaya kupitia duka hili." Alisema.

Waziri Reister alisema, kampuni ya Bevco Limited ya Ufaransa wapo tayari kushirikiana na Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA,) katika kufikia viwango vya juu vya usafirishaji kimataifa katika ukanda wa Bara la Afrika.

Aidha ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji kwa wafanyabishara kutoka nchini Ufaransa waliowekeza  nchini.

Kwa upande wake Waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alisema, wafanyabishara katika viwanja vya ndege wanaheshimiwa na kupewa fursa na kuongeza kuwa nafasi zaidi kwa wawekezaji bado zipo.

Amesema, licha ya uwepo wa changamoto ya mlipuko wa virusi vya Uviko-19 Biashara imeanza kurejea katika hali ya kawaida na wageni kutoka Ufaransa na mataifa mengine wanakaribishwa kwa shughuli za uwekezaji na Utalii.

Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Vivutio vya Kiuchumi wa Ufaransa Franck Reister akiwa ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika duka laAelia Duty Free lililopo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal III.
Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Vivutio vya Kiuchumi wa Ufaransa Franck Reister akikata utepe na kugawa kwa viongozi wa Serikali ya Tanzania na Ufaransa kama ishara ya kumbukumbu na kuenzi uhusiano uliopo baina ya Mataifa hayo.


Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...