Wanafunzi wa shule ya msingi  Kizinga  iliyopo Mbagala Kizuiani Wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam, Ramadhani Juma na Fatuma Athuman  wakipokea makopo ya rangi aina ya Coral Paints kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya  hiyo  Jokate Mwegelo,zilizotolewa msaada na kampuni ya Coral Paints  zenye thamani ya sh 15milioni  katika juhudi za kumuunga mkono  Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya kufundishia Shuleni. Kulia ni Mkuu wa masoko wa kampuni hiyo Adam Kefa.


Na Mwandishi wetu

MKUU wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo leo amepokea msaada wa rangi zenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka Coral Paints kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi ya Kizinga, iliyopo Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo, Mwegelo ameipongeza kampuni ya Insignia Limited inayozalisha rangi hizo kwa msaada huo wenye lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia shuleni hapo.

“Mmefanya jambo jema sana katika kuunga mkoni jitihada za Raisi Samia Sululhu Hassan za kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma katika mazingira bora bila changamoto yoyote,” alisema Jokate.

Awali, mkuu wa shule hiyo, John Kaula alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa majengo, hivyo msaada huo utaufanya shule hiyo ipendeze zaidi na kutoa ari kwa wanafunzi wake ya kujifunza zaidi. 

Naye Constantia Emmanuel, Afisa Elimu, Vifaa na Takwimu wa wilaya ya Temeke ameishukuru kampuni hiyo kwa kujibu maombi yao ya uhitaji wa ukarabati wa shule hiyo.

“Tulivyowafuata na kuwapa maombi yetu hamkusita na kuamua kutuunga mkono katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini,” alisema.

Baada ya kupokea msaada huo katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wanafunzi wa shule hiyo, DC Jokate alitoa maagizo kwa kamati ya shule hiyo kusimamia vema msaada huo na kuanza ukarabati wakati wa likizo ya mwezi Desemba wanafunzi wakiwa majumbani na kuanza mwaka mpya na muonekano mpya wa shule yao.

Jokate alikabidhiwa msaada huo na Adam Kefa, mkuu wa kitengo cha Masoko wa kampuni hiyo ambaye alisema wamefanya hivyo katika kumuunga mkono Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya shule hiyo wakati serikali pia ikitekeleza mahitaji mengine kama vile ujenzi wa madawati.

Mmoja wa wanafunzi hao, Sudi Hamidu anayesoma darasa la sita, kwa niaba ya wanafunzi wenzake,  ameishukuru kampuni hiyo na kusema shule yao sasa itakuwa na muonekano mzuri zaidi wenye kuvutia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...