Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewaagiza watendaji wa Wizara na taasisi zitakazotekeleza miradi ya fedha za mpango wa maendeleo  kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya uvico 19, hadi kufikia Oktoba 30, 2021 wawe wamekamilisha mpango na maandalizi ya utelelezaji wa miradi hiyo.

Waziri Prof Ndalichako ameyabainisha hayo leo  jijini Dodoma wakati akitoa mchanganuo wa fedha zitakazotekeleza miradi ya fedha hizo miradi ambayo ipo chini ya Wizara ya Elimu ambapo amebainisha kuwa kwa sekta ya Elimu imetengewa bilioni 368.9 na Wizara ya Elimu imepata shilingi bilioni 64.9 kutekeleza miradi iliyochini ya Wizara hiyo.

Ambapo Waziri Ndalichako amesema hadi ifikapo Oktoba 30, 2021 kila taasisi itakayotekeleza mradi huo iwe imekamilisha maandalizi na mipango ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango kazi utakao ainisha hatua mbalimbali za taratibu za manunuzi ya huduma na vifaa.

“Hadi tarehe 30 mwezi huu kila taasisi iwe imekamilisha na iainishe lini vifaa vitanunuliwa, vifaa vyote vinunuliwe kwa kuzingatia bei ya soko nataka na mimi nikienda kununua kifaa bei iwe ndio hiyo” amesema Prof Ndalichako.

Aidha ameagiza miradi hiyo kuhakikisha inakamilika kabla au ifikapo Mei 30, 2022 na kusisitiza matokeo ya utekelezaji wa mradi yaendane na thamani ya fedha zilizotolewa na si vinginevyo.

Ameongeza kuwa “Namuagiza Katibu Mkuu wa Wizara aandae mfumo wa uratibu, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi utakao wezesha kubaini changamoto zitakazo kuwa zikijitokeza na kuchukua hatua stahiki na kwa wakati” amesema.

Pia ametahadharisha kwamba fedha hizo hazihusishi ulipanaji wa posho ya aina yoyote na viongozi wa taasisi zinazohusika na kwamba yeye atafuatilia kwa ukaribu katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Amebainisha kuwa fedha hizo zitakwenda kuimarisha ufundishaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo shilingi bilioni 1.47 zimetengwa, kuimarisha elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stedi ambapo kiasi cha shilingi bilioni 57.98 zimetengwa na kuimarisha mazingira ya utoaji elimu ya ualimu ambapo kiasi cha shilingi bilioni 5.44 zimetengwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...