Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) Ummy Mwalimu akizungumza mbele ya wadau kutoka AZAKI wakati akifunga Wiki ya AZAKI iliyofanyika Jijini Dodoma.


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI )Ummy Mwalimu ameshiriki hafla ya kuhitimisha Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) Jijini Dodoma  na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

Pia ameshauri mashirika hayo  kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa ni moja ya mchango mkubwa wa maendeleo ya nchi na kwamba kwa kutambua mchango wao ametoa mwito kuendelea kushirikiana na  Serikali kuihudumia jamii.

Aidha ametoa mwito kwa sekta binafsi kuwekeza kwenye mashirika ya Asasi za Kiraia ili kuchangia ukuaji wa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla na kwamba kwa kufanya hivyo kutaisaidia Sekta Binafsi  kutimiza malengo yao ya huduma za jamii kwani asasi hizo zimekuwa zikifanyakazi na jamii hizo kwenye maeneo yao.

Amezitaka Asasi za Kiraia kuongeza nguvu katika suala zima la kutoa elimu kwa wananchi na kuwajengea uwezo ili wananchi hao waweze kujisimamia katika shughuli zao za kimaendeleo na kiuchumi huku akiwataka kuwasaidia madiwani kwenye halmashauri kwa  kuwajengea uwezo kwenye masuala mbalimbali yakiwemo usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo.

“Napenda kuwapongeza sana kwa elimu mnayotoa kwa wananchi kwa kuwajengea uwezo, lakini naomba muende mbali zaidi kuyafikia mabaraza ya madiwani kwenye halmauri zetu ili nao wajengewe uwezo wa kusimamia halmashauri kwenye matumizi ya fedha na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo” Ameongeza Mhe. Ummy.

 Awali akitoa Salamu na kuelezea shughuli  zilizofanywa na asasi ya kiraia kwenye Wiki ya Azaki,Mratibu wa Wiki ya Azaki na Mshauri wa Foundation for Civil Society (FCS) Justice Rutenge ameeleza kazi zilizofanywa katika wiki ya Azaki ikiwa ni pamoja na mijadala iliyowakutanisha wadau wa Asasi za Kiraia, Wabunge, Makundi Maaalum na wananchi ambapo kwa pamoja waliweza kushirikiana katika mazungumzo na mijadala iliyolenga kujadili masuala yanayohusu  ustawi wa  nchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

“Mheshimiwa Waziri Wiki ya Azaki mwaka huu imeweza kuzikutanisha Asasi zaidiya 300 ambao kwapamoja waliweza kukutana hapa Dodoma kuanzia siku ya ufunguzi na baadae kushiriki kwenye mijadala mbalimbali iliyowawezesha kutoa mawazo yao juu ya masuala mbalimbali ya ustawi wa jamii na Taifa kwa ujumla" Amesema Justice.

Wiki ya AZAKI ni jukwaa pekee nchini lililowaleta kwa pamoja  wadau wakuu wa maendeleo  ikiwemo Serikali, Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia,  pamoja na wananchi kwa lengo la  kujadili masuala yanayohusu  ustawi wa  nchi na maendeleo ya Taifa ambapo yalizinduliwa rasmi leo Octoba 23 na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai (Mb), na kufungwa rasmi leo Octoba 28, 2021.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...