Na: Projestus Binamungu

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dodoma.

Serikali imetoa wito kwa wasanii kuendelea kusajili kazi zao katika mamlaka zinazo husika ili zilindwe kisheria na malaka hizo katika kuhakikisha zinawanufaisha na kufanikisha ndoto zao.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa leo Okitoba 25, 2021, wakati akijibu maswali ya baadhi ya Wabunge waliotaka kujua msimamo wa Serikali katika kuthibiti wizi wa kazi za Sanaa kupitia ombwe kubwa la uwepo wa teknolojia zinazo wawezesha wezi kudurufu kazi za wasanii na kuziuza bila kibali cha msanii husika.

Katika kikao hicho baina ya watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Waziri Bashungwa amewaelezea wajumbe kuwa nia ya Serikali ni kuona vijana wananufaika kupitia kazi zao , lakini kwa kufuata Sheria za nchi, Kanuni, Taratibu na Miongozo zilizowekwa kwa lengo la kulinda masilahi yao.

“Kwa hiyo ndugu zangu wajumbe tuendelee kusaidizana kuwahimiza hawa vijana wetu kila mmoja kwa nafasi yake kwamba ni muhimu kusajili kazi zao katika malaka husika, ili linapotokea suala la kuibiwa kazi tuwe na meno na sehemu ya kuanzia kisheria katika kufuatilia haki ya msanii husika” amesema Waziri Basungwa mbele ya kamati hiyo ya Bunge.

Awali Katibu Mkuu wa Wizira ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara hiyo inaendelea na uratibu kuona namna bora inavyoweza kuwapeleka wataalamu wa sanaa nje ya nchi kujifunza na kuongeza ujuzi zaidi ili baadae warejee hapa nchini kuwasaidia wasanii na hasa wasanii wachanga kuzalisha kazi zenye ubora zaidi.

Akizungumza kabla ya kuhairisha kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Aloyce Kamamba amepongeza hatua zinazo fanywa na Wizara ya Utamadunia, Sanaa na Michezo ikiwa ni pamoja na hatua ya kuwezesha kutengwa kwa asilimia tano ya mapato kutoka kwenye michezo ya kubahatisha ambayo inaiwezesha Wizara kupata fedha kiasi cha shilingi Milioni 400 kwa kila robo ya mwaka kutokana na asilimia hiyo.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akijibu maswali ya baadhi ya wabunge wakati wa kikao kati ya watendaji wa Wizara yake na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizira ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Aloyce Kamamba akisisitiza jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma, na Maendeleo ya Jamii katika kikao na watendaji wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo leo Oktoba 25, 2021 Bungeni jijini Dodoma.

********************************

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...