Na Said Mwishehe, Michuzi TV
TAASISI
ya Teknolojia Dar es Salaam(DIT) imeweka wazi mikakati mbalimbali iliyowekwa
kuutekeleza mradi wa RAFIC utaokwenda kuwezesha Watanzania wengi zaidi bila
kujali viwango vyao vya elimu kupatiwa mafunzo ya kuwa na uelewa kuhusu masuala
ya TEHAMA yakiwemo ya kutumia mitandao ya simu za mkononi.
Kupitia
mradi huo wa RAFIC ,DIT imepatiwa Dola za Marekani milioni 16.25 ambazo ni sawa
na Sh.bilioni 37 ili kuutekeleza mradi huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha
miaka mitano.DIT imeamua kutumia mradi huo kujikita katika utoaji elimu na
ujuzi katika TEHAMA na lengo lao ni kuwa wabobezi katika ukanda wa Afrika
Mashariki na Afrika kwa ujumla na uwezo huo wanao kwani wanaowakufunzi wabobezi
katika mambo ya TEHAMA.
Wakizungumza
wakati wa semina maalumu iliyoandaliwa DIT kwa waandishi kutoka vyombo
mbalimbali vya habari , Waratibu wa mradi huo wa RAFIC Dk.Joseph Matiko na Daud
Mbomba wakiongozwa na Mkuu wa DIT Profesa Preksedis Marco wamefafanua kwa kina
kuhusu mradi huo ambao mchakato wake upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji
na unakwenda vizuri.
Akifafafanua
kuhusu mradi wa RAFIC, Profesa Marco amesema kuwa mchakato wa mradi huo ulianza
mwaka 2019 lakini fedha za kuanza utekelezaji zilitolewa mwaka 2020, na DIT wao
wamechukua eneo la eneo la TEHAMA na kiasi cha fedha Sh.milioni 37(dola milioni
16.25) zitatumika kwa muda wote wa utekelezaji ambao ni wa miaka mitano.
"Thamani
ya mradi ni dola za Marekani milioni 75 na fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya
Dunia na unalenga kusaidia zetu katika kuendeleza kutoa ujuzi kwa
watanzania.Mbali ya sisi DIT kupata hizi fedha , pia kuna taasisi nyingine tatu
nazo zimepatiwa kiasi sawa ambacho DIT tumapata cha dola za Marekani milioni
16.25(sawa na Sh.bilioni 37),"amesisitiza.
Awali
akielezea mradi huo, Mratibu wa RAFIC Dk.Matiko amesema taasisi hiyo imekuwa na
mipango mikubwa ya kuhakikisha wanakuwa wa kimataifa na huko ndiko ambako
wamekwenda na kwamba wameweka mipango ya miaka 100 lakini kikubwa ambacho
kinaleta furaha ni kuona kasi waliyonayo katika kukimbia ili kutatua changamoto
zinazoikabili jamii."Kwa sasa kupitia mradi wa RAFIC hapa DIT tumamua
kujikita katika TEHAMA,tunacho kituo cha umahiri wa TEHAMA ambacho kinaitwa
RAFIC.
"Pamoja
na mambo mengine kwetu hapa DIT mojawapo la eneo la kimkakati tunataka kuwa
watalaam wa Cyber Crim(uhalifu mtandaoni) tunajua Serikali imehamia katika
mifumo ya kidigijitali , ukusanyaji wa mapato unafanyika mtandaoni, DIT
tunataka kuwa na askari ambao watapambana kuulinda mfumo wa kidigitali na tuko
tayari kwa hilo.
"Kwa
hiyo tutahudumia hapa nchini na Afrika Mashariki, kwa hiyo tunaendelea na huo
mradi wa RAFIC pamoja na miradi mingine mingi. Nisisitize mradi wa RAFIC unalenga
kuendeleza ujuzi, kwa malengo ya mradi kikanda lengo la kwanza ni kuongeza
udahili, tuwe tunadahili wanafunzi wengi na lengo la pili hao wanaofundishwa
waweze kujiajiri.
"Wakati
lengo la tatu wanafunzi wetu waweze
kufanya kazi hata katika nchi nyingine, mradi huu wa RAFIC unafadhiliwa na
Benki ya Dunia, ni mradi wa kikanda, na nchi tatu zinashiriki,nchi hizo ni
Ethiopia, Kenya na Tanzania.Kwa Ethiopia unatekelezwa katika vituo saba, Kenya
vitano na kwetu unatekelezwa katika vituo vinne,"amesema Dk.Matiko.
Aidha
amesma kuna maeneo ya kimkakati ambayo Serikali imeona iwekeze, hivyo hata
mradi huo umeangalia maeneo ya mkakati, mradi huo unatekelezwa Chuo cha Ufundi
Arusha ambapo wao wamejikita katika nishati na chuo hicho kimepewa Dola za
Marekani milioni 16.25(Sh.bilioni 37.
Wakati
Kampasi ya Mwanza itajikita katika uchakati wa ngozi na imepewa kiasi cha dola
milioni 16.25, Chuo cha Usafirishaji cha Taifa(NIT)chenyewe kitajikita katika
usafirishaji wa anga na wao wamepewa dola za Marekani milioni 16.25 na wao DIT
wamejikita katika TEHAMA.
Alipoulizwa
kwanini DIT wameamua kujikita katika TEHAMA, Dk.Matiko amejibu hivi
"tuliona tujikite katika eneo la ujuzi wa kidigital, elimu ya kidigital
inahitajika sana, kwa hiyo lazima elimu hiyo ifike kwa kila mmoja wetu.Kuna
ombwe kubwa ndio maana watu wanaibiwa fedha kwenye simu, hivyo kila mtanzania
ni vema akawa na elimu ya awali kuhusi matumizi ya digitali.
"Tunaangalia
katika nyanja tatu , kwanza tunamuangalia mtu ambaye hana elimu kubwa lakini
tunataka apate elimu itakayomuwezesha kutumia vifaa vya TEHAMA kwa ufanisi,
mfano anayetumia simu.Kwa hiyo tutaangalia jamii nzima bila kuangalia viwango
vya elimu, tutakuwa na programu ambayo itatuwezesha kutoa elimu ya namna ya
kutumia mitandao ya kidigitali.
"Pili
tutaangalia ni namna gani tutaboresha mitalaa yetu, mtu yoyote bila kujali
taaluma yake awe na uelewa wa kutumia angalau Lptop kwa ajili ya masuala
yake.Pia tutaangalia viwango vya elimu na kutoa mafunzo , hivyo hakuna mtu
ambaye ataachwa.Tunakwenda huko kwasababu tuafahamu huduma nyingi zinakwenda
katika mndao, zamani cheti cha kuzaliwa ilikuwa lazima uende RITA lakini sasa
unakipata mtandaoni".
Aidha amesema katika mradi wa RAFIC kuna baadhi ya vitu wanatakiwa kufanya na mojawapo ni kupata cheti cha kutambulika kimataifa(ISO 21001) na mchakato unakwenda vizuri na matarajio yao DIT itakuwa taasisi ya kwanza kupata kupata hiyo ISO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...