Afisa Habari Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala akizungumza wakati wa uzinduzi wa Aplikesheni ya Parent Experiance, uzinduzi uliofnyika jijini Dar es Salaam. kulia Mbele ni Mkurugenzi Mkuu wa ShuleSoft, Ephraim Swilla
Mkurugenzi Mkuu wa ShuleSoft, Ephraim Swilla na Afisa Habari Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu wakisikiliza maelekezo katoka shule soft.


Baadhi ya wadau wa elimu wakiwa katika uzinduzi wa aplikesheni ya Parent Experiance iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

TAASISI isiyo ya kiserikali ya mifumo ya Teknolojia ya elimu nchini kupitia mtandao wa shulesoft imezindua aplikesheni ya ‘Parent experience’ ambayo itawashirikisha wazazi katika maendeleo ya mtoto shuleni.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Afisa Habari Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala amesema kuwa serikali inaunga mkono juhudi za vijana katika ubunifu wa kidijitali.

Amesema Shulesoft itakuwa mkombozi kwa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kupunguza matumizi ya karatasi kwani itasaidia mwanafunzi mpaka mwalimu au mkufunzi katika kujifunza masomo mbalimbali kwa njia ya kidijitali.

“Shulesoft itawezesha sekta ya elimu kufanya kazi kidijitali na kurahisisha huduma mbalimbali zinazoendelea katika sekta hiyo.” Amesema Mwakyanjala

Amesema mfumo hu utawezesha shule zote nchini katika kufuatilia wakati wa kusajili wanafunzi, kufatilia malipo, kufatilia nani hajafika shule, wazazi kufuatilia maendeleo ya mtoto akiwa shuleni, usalama wa watoto pamoja na ufuatiliaji wa usafiri wa mtoto.

Mwakyanjala amesema ShuleSoft imeleta mafanikio makubwa katika sekta ya elimu kuepukana na matumizi makubwa ya karatasi kwani inaepusha upotevu wa karatasi na kurahisisha walimu na wakufunzi kusahisha mitihani na kujaza maksi za wanafunzi kwa mfumo ambao utakuwa na kumbukumbu zote zinazohusiana na wanafunzi na walimu.

Pia amewapongeza Shulesoft kwa kutengeneza baadhi ya mifumo ya serikali ili kurahisisha kazi serikalini hasa walipo tengeneza mfumo wa kusajili biashara kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) hata hivyo amewaomba Shulesoft kuwasaidia walimu wawe na mfumo utakaowawezesha kuandaa maandalio ya somo kupitia mfumo wa kidijitali.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mkuu wa ShuleSoft, Ephraim Swilla amesema kuwa mfumo wa Shulesoft unasaidia uendeshaji wa shughuli mbalimbali katika tasisi, shule, vyuo vya kati na vyuo vikuu ili viwe na ufanisi mkubwa licha ya hayo mfumo huo utasaidia kukusanya fedha kwa urahisi zaidi.

Amesema wazo la kubuni program hiyo lilikuja baada ya kufanya tafiti mwaka 2016 katika shule mbalimbali za binafsi na za Serikali na kugundua kuwa kuna changamoto ya mawasiliano kati ya mzazi na shule.

Amesema malengo ya kuanzisha aplikesheni ya Parence experience itasaidia mzazi kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mtoto kiganjani mwake.Amesema hadi sasa shule takribani 700 zimeshajiunga katika mfumo huo hapa nchini pia vilevile baadhi ya shule kutoka nchi nyingine kama vile Madagasca na China.

Amesema aplikesheni hiyo inapatikana kwenye simu za anroids kupitia Play store na appstore kwa simu za iphone ili kumwezesha kila mzazi kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi lakini kwa wazazi wasio na simu janja shulesoft wanampango wa kutengeneza mfumo utakao wasaidiawa wazazi kupata taarifa za mtoto kwenye simu.

Swilla amesema kuwa aplikesheni hiyo inatumia lugha mbili ambazo ni Kiswahili na kingereza kwaajili ya usalam wa utoaji taarifa kwa mzazi. Pia amesema kuwa mfumo huo utasaidia shule kupunguza gharama za uendeshaji na kusaidia shule kuboresha taaluma kwa wanafunzi.

Amesema kuwa Aplikesheni hiyo itasaidia shule kukusanya fedha kwa urahisi, kusaidia shule kupunguza gharama za uendeshaji, kuboresha uandaaji wa taaluma, itasaidia shule kutengeneza namba za malipo ya ada kwa kila mwanafunzi kwa kupitia benki washirika pia kwa kulipia kwa kutumia mitandao ya simu, itasaidia kupanga matumizi ya shule, kutengeneza ripoti za shule, kuandaa matokeo ya mtoto pamoja na kuandaa mishahara kwa wafanyakazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...