Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TotalEnergies Jean-Francois Schoepp akizungumza wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa vilainishi vya kampuni hiyo na kueleza kuwa bidhaa na huduma zinazotolewa zinazingatia teknoloja ya hali ya juu na manufaa kwa watumiaji.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akzungumza katika hafla hiyo ambapo ameipongeza kampuni ya TotalEnergies kwa uwekezaji faafu nchini pamoja na kutoa ajira kwa vijana na kupanua soko kwa nchi saba zaidi barani Afrika, Leo jijini Dar es Salaam.




Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

KAMPUNI ya mafuta ya TotalEnergies Tanzania imezindua mwonekano mpya wa bidhaa za vilainishi katika mwonekano wa vifungashio vya vilainishi hivyo kwa teknolojia ya juu ambayo imechangiwa na teknolojia ya vijana wa kitanzania ikiwa ni sehemu ya kutoa huduma bora kwa wateja kulingana na mahitaji yao pamoja na kuimarisha uhalisia wa bidhaa za kampuni hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesema, kampuni hiyo imekuwa ikitumia ubunifu na teknolojia ya juu katika uzalishaji wa bidhaa zake ambazo kwa sasa zinazalishwa hapa nchini na kusambazwa katika nchi saba za Afrika ikiwa ni hatua kubwa katika maendeleo ya biashara na viwanda.

''TotalEnergies wana bidhaa zao hapa nchini na ni faafu kwa matumizi ya mashine na mitambo pamoja na vyombo vya moto, uzalishaji wa bidhaa zao hapa nchini umeleta faida kubwa kwanza ajira kwa vijana wa kitanzania na kwa kuzisambaza katika nchi jirani tunapata fedha za kigeni, mapato, soko la nje, teknolojia na kujitanua zaidi kibiashara kama azma ya Serikali ya awamu ya sita inayosimamia na kutekeleza....Na nimesikia mpango wao wa kuja na nishati ya upepo na jua naamini mkakati huu utaleta tija kwa taifa'' Amesema.

Kigahe ameishauri kampuni hiyo kuendelea kuzalisha bidhaa zenye kukidhi viwango na kuzisambaza katika bara la Afrika na duniani kwa ujumla na kueleza kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kuhakikisha lengo lao la kutoa huduma kwa teknolojia ya juu kwa watanzania linafanikiwa.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa TotalEnergies Tanzania Jean-Francois Schoepp amesema kuwa muonekano mpya wa bidhaa za vilainishi uliozinduliwa unakwenda sambamba na wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa barani Afrika na wanatumia wiki hiyo kusikiliza maoni ya wateja ili kuweza kuboresha huduma zao zaidi.

Ameeleza tangu kuanza kwa kampuni hiyo hapa Tanzania wamekuwa wakitimiza malengo ya wateja wao kupitia huduma zao ambazo zina teknolojia ya juu na isiyoghushiwa.

Pia amesema kuwa wamekuwa wakizalisha bidhaa za vilainishi hapa nchini na kusambaza katika nchi saba za Afrika hali iliyopelekea kukuwa kwa soko na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha teknolojia cha uzalishaji na usambazaji wa bidhaa hizo zinazokubaliwa ndani na nje ya nchi na ameishukuru Serikali kupitia wizara ya Viwanda na Biashara kwa ushirikiano wanaoonesha katika kuyafikia malengo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TotalEnergies Getrude Mpangile amesema mwonekano mpya wa bidhaa uliozinduliwa ni wa teknolojia ya juu na wanajivunia kwa kuwa umefanywa na vijana watanzania kupitia wataalam mbalimbali waliopewa mafunzo hapa nchini.

Amesema katika kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa nishati nchini kampuni hiyo kwa kushirikiana Serikali wana mpango wa kuzalisha nishati ya jua na upepo ili kuboresha sekta hiyo hasa katika nyanja za viwanda katika uchakataji wa bidhaa mbalimbali.


Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TotalEnergies Getrude Mpangile akizungumza na wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa muonekano mpya wa bidhaa hiyo umefanywa na vijana watanzania, Leo jijini Dar es Salaam.














Matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...