Na Khadija Kalili ,Kibaha

Meneja  wa Mamlaka ya Mapato  Mkoa wa Pwani (TRA) Godwin  Barongo amekifunga kiwanda bubu Cha mambomba ya maji kilichogundulika kuwepo katika maeneo ya Miembesaba Kata ya Kongowe Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

"Jana jioni tulipata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari kutakuwa na kikao maalumu na baada ya kufika ofisini kwake  leo asubuhi akatueleza kuwa kuna kiwanda Cha kutengeneza mambomba ya maji ambacho hakina usajili wa aina yeyote katika eneo hilo.

Tumechukua jukumu la kuja katika kiwanda hiki ambacho hakuna Ofisi, Mneja ila wapo vijana wachache ambao wamekua wakiendelea na uzalishaji wa mabomba ambayo tumeelezwa kuwa mambomba hayo hupelekwa Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

"Leo hii tutahesabu mabomba  na malighafi zote zilizomo ndani ya kiwanda hiki na baada ya  hapo  tutamwita muhusika Ili aje atuthibitishie kama yeye ni mlipa kodi halali aje na vithibitisho vyote  kama amesajiliwa licha ya kupekua  hatujapata nyaraka za aina yeyote ambazo zingetusaidia kumtambua muhusika alisema Barongo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Pwani RPC Nyigesa Wankyo alisema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema pia Mara baada ya kukagua ndani ya kiwanda hicho walikuta kiitabu kilicho andikwa Tiger Investment Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi zaidi Ili kuweza kumpata mmiliki .

Inspekta kutoka  Shirika la Viwango Tanzania (TBS ) Venance Colman alisema  amefika hapo  pamoja na Kamati  iliyoundwa na  RC  Kunenge kuwa bahati mbaya hawana nyaraka za aina zinzoonyesha jina la mzazlishaji lakini wanazalisha  mambomba ya maji hivyo sisi  tuta chukua sampuli za bidhaa zote na kwenda kuzipima  na kuangalia kama bidhaa zote zinazozalishwa kitandani  hapo zinakidhi viwango  na kama hazikidhi matakwa ya viwango hatua stahiki zitachukuliwa kwa wahusika.

Hata hivyo Mkurugenzi Jupiter Investment Vincent Meena amekanusha kuwa kiwanda hicho siyo bubu kwani wanavyo vibali vyote halali vya uendeshaji wa kiwanda na wako tayari kuviwasilisha kwa Jeshi la Polisi Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...