Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mahakama kuu kanda ya Iringa iliyokaa kupitia kikao chake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe,imewahukumu washtakiwa wawili Mwapulise Mfikwa (29) na Manase Mhada (25) kunyongwa hadi kufa kutokana na kukutwa na hatia ya kumuua Bi,Eva Merikion Mgaya (28) nyumbani kwake huko kijiji cha Ihanga wilayani Njombe.

Imeelezwa kuwa katika shauri la Jinai namba 2/2018 la mauaji ya Bi, Eva Merikion Mgayawashtakiwa hao akiwemo Mwapulise Mfikwa mbena ambaye ni mkazi wa Kibaigwa,Dodoma na Manase Mhada mbena mkazi wa Kifanya mjini Njombe,walitekeleza mauaji hayo baada ya kuvamia nyumbani kwa marehemu walipofika kwa lengo la kuiba.

Akisoma hukumu hiyo Mh.Jaji Filmin Matogolo amesema tukio la mauaji lilitokea huko katika kijiji cha Ihanga mnamo tarehe 8/5/2015 baada ya washatakiwa kwenda nyumbani kwa Wilfred Vitus Ng’olo ambaye ni mume wa marehemu wakiwa na siraha aina ya bunduki shotgun iliyotengenezwa kwa njia za kienyeji inayotumia risasi aina ya 12 bore ambapo walivamia,kuiba na kunyang’anya fedha nyumbani kwa marehemu.

Mahakama imeeleza kuwa vile vile washatakiwa walifanikiwa kuchukua simu ya mume wa marehemu na kumpiga risasi Eva Merikion Mgaya kifuani kwa kutumia bunduki hiyo na kusababisha kifo chake papo hapo na kisha kutoweka mpaka walipokuja kukamatwa baada ya upelelezi juu ya mauaji hayo.

Mh.Jaji Filmin Matogolo amesema washtakiwa hao walitenda kosa kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha Kanuni ya adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2019.

Kwa upande wao mawakili wa utetezi Jerome Njiwa na Octavian Mbungali,mara baada ya hukumu hiyo wameiomba mahakama kukabidhi siraha iliyotumika kwenye mauaji kwa jeshi la polisi na simu kurudishwa kwa mume wa marehemu.

Aidha shauri hilo limeendeshwa na wakili wa serikali Adrew Mandwa pamoja Matiku Nyangero.
Watuhumiwa wakiingizwa katika  lock up ya mahakama mara baada ya kusomewa hukumu kwa ajili ya kwenda kutumikia adhabu yao.



Jengo la mahakama ya hakimu mkazi Njombe jipya lililoanza kutumika hivi karibuni mara baada ya kukamilika katika eneo la Lunyanywi mjini Njombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...