Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi ametoa wiki moja kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kuitisha kikao na vyama vyote vya michezo vilivyopo kwenye mgawanyo wa wachezaji (Quarter) kwenye Mashindano ya Madola yatakayofanyika Julai 2022 nchini Uingereza ili kusikiliza changamoto na kuwapa mwelekeo wa namna bora ya usimamizi wa michezo kuelekeza mashinda ya kimataifa.

Dkt. Abbasi ametoa maelekezo hayo leo kwenye kikao alichokiitisha leo Disemba 3, 2021 kilichoshirikisha Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo, Baraza la Michezo la Taifa, Baraza la Michezo la Majeshi na Kamati ya Olympic ya Tanzania (TOC) ili kupokea taarifa ya TOC na Mpango kazi wa maandalizi ya timu za taifa kuelekea maandalizi ya ushiriki wa Michezo ya Jumuiya ya Madola.

Aidha, wajumbe wameiomba Serikali kutupia macho kwenye baadhi ya vyama vya michezo visivyofuata utawala bora ili kuwafanya wachezaji kufanya vizuri.

Akizungumzia maendeleo ya michezo nchini, amesema kwa sasa ni muhimu kuchagua michezo michache ya kimkakati inayofanya vizuri ili kupata mafanikio.

Aidha, Dkt. Abbasi amefafanua kwamba ili kuendeleza michezo nchini ni muhimu kwa wadau hao kubuni vyanzo vya uhakika mapato vitakavyotoa fedha kwa ajili ya kuendeshea shughuli za michezo.

“Tunatarajia kuanza makambi ya michezo mapema ili kujiandaa na michezo ya kimataifa”. Amesisitiza Dkt. Abbasi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...