Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua kampeni hiyo na kueleza kuwa wataendelea kuwafikia wananchi kwa kuwajengea utamaduni wa kufanya usafi ili kuiweka Wilaya na Mkoa wa Dar es Salaam katika hali ya usafi.







MKUU Wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amesema kuwa hawatamlazimisha mtu kufanya usafi ila zoezi hilo litakuwa shirikishi na endelevu kwa Wilaya hiyo katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama ndani ya Wilaya hiyo na jiji kwa ujumla.

DC Jokate ameyasema hayo leo wakati akizindua kampeni ya siku ya usafi kwa ngazi ya Wilaya, Kata na mitaa, Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa kampeni hiyo maalum ni endelevu kwa wananchi kufanya usafi kila jumamosi na mwisho wa mwezi pia wameungana na Mkuu wa Mkoa huo Amos Makalla aliyeanzisha kampeni hiyo kwa kauli mbiu ya 'Safisha, Pendezesha Dar es Salaam'

''Hii sio kampeni ya siku moja na hatulazimishi mtu kufanya usafi wala kuwa na muda maalum wa kufanya usafi ukiamka fanya usafi endelea na shughuli nyingine, tumetengeneza mazingira ya watu kuona wajibu wao katika kushiriki katika hili, Mwamko ni mkubwa vijana, wananfunzi na wadau mbalimbali wamejitokeza kwa wingi katika zoezi hili na tutatembea na kauli mbiu ya ;Safisha, Pendezesha Temeke.' Amesema.

Amesema mazingira ya maeneo ya Wilaya hiyo ikiwemo Mbagala yanavutia na wataendelea kuwajengea wananchi utamaduni huo wa kusafisha mazingira.

Aidha amesema kuwa wameungana na Mkuu wa Mkoa katika kampeni hiyo na wamehamasisha wafanyabiashara kusafisha katika maeneo yao ya kazi na watapita katika mitaa na kata na kuwahimiza wananchi kushiriki shughuli za usafi wao binafsi na usafi wa mazingira na kuwajengea utamaduni wa kufanya usafi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya amesema zoezi hilo ni endelevu kwa mujibu wa agizo la Mkuu wa Mkoa huo kwa kuwataka wananchi kufanya usafi kila mwisho wa mwezi na Wilaya hiyo imejipanga na watatekeleza agizo hilo.

''Wilaya ya Temeke imejipanga katika kufanikisha zoezi hili kuna vifaa vya kutosha na katika bajeti ijayo tutaongeza bajeti, Nawaomba wakazi wa Temeke tushirikiane katika kufanikisha zoezi hili kwa kuwa Temeke inawezekana bila uchafu.'' Amesema.

Amesema,mwamko na ushirikiano iliooneshwa na wanafunzi, vijana na vikundi mbalimbali ni dhahiri kwamba kampeni hiyo itafanikiwa na uongozi wa Wilaya hiyo utaendelea kuwa karibu na wananchi na kuwajengea utamaduni ya akufanya usafi.

Kampeni hiyo imehudhuriwa na viongozi wa kata na mitaa ya Wilaya hiyo, Madiwani,vijana, wanafunzi, DAWASA Temeke, TANROAD Mkoa, Jeshi la Uhamiaji, na wakati wa Kibonde Maji, Mbagala Kuu, Charambe na Mianzini.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni na kueleza kuwa Temeke bila uchafu inawezekana na wamejipanga kuongeza bajeti ya vifaa vya usafi ili kufanikisha kampeni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
















Matukio mbalimbali katika picha wakati wa kampeni ya usafi ya 'Safisha Pendezesha Dar es Salaam.'


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...