Na Amiri Kilagalila,Njombe


MAHAKAMA ya wilaya ya Njombe imemuhukumu Bright Peter Dismas (25) mkazi wa Kitisi halmashauri ya mji wa Makambako kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili likiwemo la ubakaji na kumpa ujauzito mwanafunzi.

Hukumu hiyo imetolewa leo na hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Njombe Isack Mlowe ambapo amesema mshtakiwa huyo alimbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 17 wa shule ya sekondari Mkilima iliyopo mjini Makambako.

Alisema tukio hilo la ubakaji lilitokea mwaka jana mwezi Februari katika mtaa wa Kitisi halmashauri ya mji Makambako.

Amesema mshtakiwa alianzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo ambapo siku ya tukio alikwenda nyumbani kwao akiwa peke yake.

Amesema baada ya kufika nyumbani hapo mshtakiwa huyo aliingia ndani na kuandaliwa chakula na mwanafunzi huyo kisha baadae wote wakaenda chumbani na kufanya mapenzi.

Amesema ilipofika mwezi oktoba mwaka jana mwanafunzi huyo aligundulika kuwa na ujauzito baada ya kufanyika vipimo shuleni kwa wanafunzi wote wa kike.

"Mwanafunzi huyo baada ya kugundulika kuwa na ujauzito alihojiwa ndipo akaeleza mahusiano yake na mshtakiwa" alisema Mlowe.

Amesema mshtakiwa huyo alihukumiwa kulipa fidia ya shilingi 1,000,000/= kama fidia kwa mwanafunzi huyo baada ya kutoka gerezani.

Wakili wa serikali Matiko Nyangero aliyekuwa akiendesha shauri hilo la jinai Namba 198/2020 aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na katika kutoa adhabu izingatie matakwa ya kifungu cha 130 (1) (2) (e) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya 2019, ambavyo mshtakiwa ameshtakiwa navyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...