Tarehe 5 Desemba 2021  itakuwa imetimia miaka 20 tangu Brig. Jen (Rtd) Moses Nnauye, ambaye alishika nyadhifa mbalimbali kwenye taasisi tofauti ikiwemo Serikali, Jeshi, Chama cha Mapinduzi n.k., alivyoaga dunia. 

Alifariki dunia kwenye hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo, Dar es Salaam na kuzikwa makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, tarehe 7, Desemba, 2001, siku mbili kabla ya sherehe za miaka 40 ya Uhuru wa Tanganyika na miaka 39 ya Jamhuri ya Tanzania Bara. Ili kufanya kumbukizi na kuenzi utumishi na mchango wake kupitia taasisi mbalimbali ambazo aliwahi kuhusika nazo kikazi wakati wa uhai wake, familia ya hayati Brig. Jen (Rtd) Moses Nnauye ikiongozwa na mjane wake Mama Mwanaisha Nnauye wameandaa kumbukizi itakayokuwa na matukio mawili yafuatayo: 

1. Mjadala mfupi kuhusu ninavyomfahamu Marehemu Brig. Gen (Mstaafu) Moses Nnauye utumishi wake na mchango wake kwa nchi yetu. Mjadala huo utafanyika katika Ukumbi wa JNICC uliopo mtaa wa Shaaban Robert tarehe 5 Desemba 2021, kuanzia Saa tatu (3:00)asub mpaka saa saba (7:00) mchana.

2. Hitma ambayo itafanyika katika kijiji cha Chiuta, tarafa ya Nyamangana, Wilaya ya Lindi Vijijini, mkoa wa Lindi. Hitma itafanyika kwenye tarehe  16 Desemba 2021. 

Familia itachukua nafasi hiyo pia kukumbuka na kuzingatia urithi aliouacha wa mfumo wa maisha yake ya upendo, uadilifu, uvumilivu pamoja na moyo wa kujitoa kwa wenzake na taifa kwa ujumla. 

Familia imetoa mialiko mbalimbali kwa viongozi wa Chama na Serikali, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, akiwemo Rais Mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete wanamichezo na wanasanaa, jamaa na marafiki ili kuhudhuria matukio haya mawili aidha kwa pamoja au mojawapo. 

Imetolewa na:

Familia ya Brig. Gen (Mstaafu) Moses Nnauye

03/12/2021

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...