Na Woinde Shizza,Arusha


MKUU wa mkoa wa Arusha John Mongela ameyaomba madhehebu ya dini kushikamana na serikali katika kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa UKIMWI kwani ugonjwa huo bado ni changamoto katika jamii.

Mongela alitoa ombi hilo katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyoadhimishwa kiwilaya katika eneo la Kilombero mkoani Arusha ambapo alisema kuwa ni vema madhehebu ya dini yakaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kupambana na UKIMWI.

Alifafanua kuwa madhebu ya dini yana programu mbalimbali za kusaidia hivyo Wana haja ya kuendelea kushikamana ili mafanikio yaweze kuwa makubwa lakini pia serikali inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na madhehebu ya dini katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Sambamba na hayo pia aliitaka jamii kuunga mkono suala la kupima, kujua afya zao, na kufuata masharti ya kujikinga na maambukizi lakini pia Kuacha tabia za kizamani za unyanyapaa kwani kwa sasa hivi mtu mwenye maambukizi anamchango sawa au zaidi ya yule ambaye hana maambukizi.


Kwa upande wake Tajieli Mahenga kaimu afisa maendeleo ya jamii jiji la Arusha alisema kuwa kwa mwaka 2021 wameweza kuelimisha kata zote 25 za jiji la Arusha juu ya maambukizi na namna ya kujikinga na maambukizi hayo , kugawa Kondom za kike na kiume laki 9 na 80 huku watu laki 3 na 70 mia 603 wameweza kujitokeza kupima afya zao na wenye maambukizi wapatao 2150 wameingizwa kwenye tiba na matunzo katika vituo vya afya vya jiji la Arusha.


Alifafanua kuwa wameweza kuongeza vituo vya klinik kutoka 17 hadi 22 pamoja na kiwango cha kufubaza UKIMWI kimeongezeka kutoka asilimia 85 hadi 95 ambapo pamoja na mafanikio hayo pia wanakabiliwa na changamoto ya kiwango cha maambukizi ya UKIMWI kuongezeka kutoka asilimia 2.3 mwaka 2019/2020 hadi kufikia asilimia 2.8 2020/2021.


“Kiwango hiki kinaongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upimaji wa makundi maalum ambayo ni vijana walioathirika na madawa ya kulevya, madada poa na makundi mengine huku nyingine ikiwa ni kuzingatia vigezo vya upimaji ambao umeongeza ufanisi wa upimaji na watu wengi wamehamasika kujijitokeza kupima,”Alisema Tajieli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...