RAIS Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewatunukia wahitimu 1,114 wa shahada na stashahada mbalimbali za Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) katika mahafali ya 15 ya Chuo hicho.

Wahitimu 431 sawa na asilimia 38.7 ni wanawake ambapo ya Chuo hicho ni kuona usawa wa asilimia kati ya wahitimu wa kike na wa kiume.

Akizungumza wakati wa mahafali ya 15 ya MUHAS, Kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi , Dkt Kikwete amesema Chuo cha Muhas kitaendelea kubaki katika historia ya maisha yake kwa sababu aliweza kupigania kuhakikisha kinajitosheleza kwa kila kitu.

Amesema, akiwa Rais alihakikisha Muhas wanapata eneo lao ambalo wanaweza kujenga Chuo na Hospitali ili wataalamu wa fani mbalimbali.

“Mara ya mwisho nilifika hapa wakati natunukiwa PHD kwa mchango wangu mkubwa nilioufanya katika sekta ya afya, ila leo nimekuja kwa niaba ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye amepata dharura,” amesema

Makamu Mkuu wa Chuo cha Muhas Prof Andrea Pembe amesema Muhas bado chuo chao kina changamoto kubwa katika udahili wa wanafunzi kutokana na uhaba wa miundo mbinu ya kutosha na Wanaendelea na juhudi za ujenzi katika kampasi ya Mloganzila na upatikanaji wa rasilimali watu wa kutosha.


“ jumla ya wanafunzi 848 wamefanikiwa kudahiliwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 4 kutoka kwa wanafunzi waliodahiliwa mwaka jana katika shahada ya kwanza  na wanafunzi 3297 waliomba na wenye sifa za kujiunga na Shahada ya kwanza ya udaktari wa Binadamu ni 230,”amesema Prof Pembe.

Amesema, katika kuzingatia umuhimu wa kuongeza wataalamu wa afya kwenye fani mbalimbali kulingana na mahitaji ya soko la ajira, Muhas wamefanikiwa kudahili wanafunzi 30 kwenye programu moja mpya ya shahada ya kwanza ya Fiziotherapia baada ya kupata ithibati toka Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU).

Aidha katika wahitimu wa mwaka huu, wahitimu 4 wametunukiwa Shahada ya uzamivu  na wahitimu 20 wakitunikiwa Digrii ya Uzamilizi na Utaalamu .

Wahitimu 201 wametunukiwa stashahada ya juu katika fani mbalimbali za afya na sayansi Shirikishi, wahitimu 535 watapata shahada ya kwanza na wengine 354 shahada ya uzamili.
Sehemu ya wanafunzi walio hitimu mafunzo mbalimbali MUHAS
Maandamano ya Kuingia katika Viwanja vya Muhimbili kwa ajili ya Kuanza kwa Mahafali ya 15 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Wahitimu wa Shahada ya Uzamivu (PHD) wakiwa wamesimama mbele ya Mgeni wa Chuo Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kutunukiwa Shahada zao kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)

Picha ya Pamoja ya Mgeni wa Chuo, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) baada ya kutamatika kwa  mahafali ya 15 ya Chuo hicho

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...