Na. John Mapepele
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ameipongeza Timu ya Taifa ya Walemavu ya Mpira wa Miguu (Tembo Warriors) kwa kufuzu Kombe la Dunia nchini Uturuki Oktoba 2022.
"Nawapongeza viongozi wa Wizara na TFF na nawataka mfanye maandalizi mazuri zaidi kuelekea michuano hiyo ili tuwe na timu bora itakayotutangaza vyema". imesema taarifa aliyoitoa Mhe. Rais kwenye mtandao wake wa Twitter.
Naye, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa leo akiwa jijini Mbeya ameipongeza Timu ya Tembo kwa kufuzu kuingia kwenye mashindano ya Dunia.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ameongoza watanzania kuwapa hamasa wachezaji wakati wa mechi hiyo amewapongeza wachezaji na Kamati maalum aliyoiteua kuratibu iliyokuwa inasimamiwa na Katibu Mkuu wa Wizara yake Dkt. Hassan Abbasi.
Akizungumza na wachezaji mara baada ya kushinda mechi ya kufuzu dhidi ya Cameroon magoli 5-0 Mhe. Bashungwa amesema Serikali itaendelea kuisaidia timu hiyo ili kuhakikisha inaendelea kulilitea heshima taifa katika mashindano ya dunia yanayokuja.
Kwa upande wake Dkt. Hassan Abbasi amesema amefurahishwa na hatua ya timu hiyo kazi iliyobaki ni kuhakikisha kombe hilo la CANAF 2021 linabaki Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...