NAIBU Waziri afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto bi.mwanaidi ally khamis amesema serikali itabeba jukumu la kuwasomesha watoto na kuwalea walionusurika kifo baada ya mama yao mzazi kunywesha sumu.

Amesema serikali itachukua jukumu  hilo kuanzia sasa hadi watakapopata uwezo wa kujitegemea lakini ni lazima wapewe msaada wa kisaikolojia.

Amewataaka maafisa ustawi wa jamii kutokukaa  ofisini pekee take badala yake wazungukie wananchi na kuwasaidia wale wanaopitia matatizo ya kiuchumi na kisaokolojia kuokoa maisha yao.

Amesema ingawa mama watoto hao bi.Veronica anajutia kitendo hicho, ni lazima sheria ifuate mkondo wake na atakapokuwa gerezani basi ustawi wa jamii wawajibike kumupa msaada wa kisaikolojia.

Pia ameomba jamii kujenga utamaduni wa kusaidiana pale mmoja anapopitia maisha magumu na kurejesha maisha ya upendo na kupunguza matukio ya kikatili kama hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemery Senyamule amesema tayari watoto watatu walionusurika wamechukuliwa na kupelekwa kituo cha kulelea watoto Cha Moyo wa Huruma na kituo cha neema house mjini Geita

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema Veronica anaendelea kushikiliwa mahabusu ya wilaya ya Chato na atafikishwa mahakamani wiki ijayo.

Kamanda Mwaibambe amesema Veronica anatuhumiwa kwa makosa matatu ambayo ni kuua kwa kukusudia, kujaribu kujiua na kujaribu kukatisha maisha ya watu wengine (watoto wake).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...