Muandaaji wa Tamasha la Waokaji Keki  Manka Rajab ameeleza lengo la kuandaa Tamasha hilo ni kupanua biashara ya keki na kuwakutanisha Waokaji kutoka sehemu mbalimbali Ili kupeana na kubadilishana ujuzi

  

Na Khadija Seif, Michuzi Tv

TAMASHA La Waokaji wa keki kukutanisha walaji keki,wapishi na wajasiriamali wa biashara ya Keki kupatiwa semina ili kuwajengea uwezo wa kuiona fursa ya kujitanua kimasoko katika biashara hiyo.

Akizungumza na Michuzi Muandaaji wa Tamasha la Waokaji Jijini Dar es salaam Manka Rajab amesema Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika disemba 12 mwaka huu katika ukumbi wa Hekima uliopo Mikocheni jijini Dar es salaam na kutarajiwa kuhududhuriwa na watu mbalimbali ikiwemo Waokaji kutoka Mikoa tofauti tofauti.

"Kwa mara ya kwanza tunafanya Tamasha letu na litafanyika katika ukumbi wa Hekima uliopo Mikocheni tunategemea tutapeana na kujuzana mengi katika Tamasha letu ikiwemo kupika keki mubashara na kutayarisha vifaa vya uokaji vitafunwa na keki kwa wapishi ambao tayari wamejisajiri kushiriki Tamasha letu".

Hata hivyo Manka ameeleza zaidi lengo la kuandaa Tamasha la Waokaji Kwa mara ya kwanza na kupatiwa Semina Kwa wapishi hao.

" Tamasha letu linalenga kuwakutanisha Waokaji sehemu mbalimbali na watapatiwa Semina elekezi Ili kupeana maarifa zaidi ya kuboresha biashara hiyo,namna ya kutafuta wateja na kubadilishana  ujuzi".

Pia ameongeza kuwa muitikio mzuri na tayari maandalizi ya Tamasha hilo linaendelea vizuri na takribani washiriki 60 wameshachukua fomu za ushiriki  Huku akiwaomba wadau kujitokeza Kwa wingi katika Tamasha hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...