Na Amiri Kilagalila,Njombe


Baadhi ya wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe,Njombe Press Club (NPC) kwa kushirikiana na baadhi ya waandishi kutoka mkoa jirani wa Ruvuma. Wamefanya ziara ya kutembelea hifadhi ya Kitulo iliyopo wilayani Makete ikiwa ni sehemu ya kujifunza na kutangaza utalii wa ndani.

Mapema Disemba 5 2021 wanachama wapatao zaidi ya 35 wameshiriki safari hiyo ya kutangaza utalii kutoka vyombo vya habari mbalimbali vya mkoa wa Njombe na Nje ya Mkoa wa Njombe.

Awali viongozi wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe NPC akiwemo Nickson Mahundi mwenyekiti wa NPC na katibu wa NPC Hamis Kassapa wamewaeleza waandishi wa habari kuwa hifadhi ya Kitulo ina vivutio vingi hivyo ni nafasi pekee waliopata waandishi hao kwa pamoja kushiriki kutembelea hifadhi hiyo na kujifunza.

"Waandishi wa habari nawasihi zinapotokea fursa kama hizi za kufanya tour ni vizuri kila mmoja kushiriki kuna mengi yakujifunza,kwa sababu inawezekana peke yako usingeweza kufanya ziara kama hii,huku kuna ndege ambao ni nchi chache sana duniani zinazoweza kuwaona sisi tutawaona sababu ndio miezi yao kuwa nchini Tanzania"amesema Kassapa.

Waandishi hao walipokelewa na kaimu mhifadhi mkuu Bw.Jackson Shirima ambaye alieleza kufurahishwa na safari ya waandishi wa habari kufika kutalii na kuwaomba wawe mabalozi wa utalii wa hifadhi hiyo,kisha kuwapa elimu ya mtalii awapo hifadhini ikiwa ni pamoja na kutokupiga kelele hifadhini,kunywa au kuogelea katika maji yaliyoko katika hifadhi hiyo pamoja na kutotupa taka yoyote katika hifadhi ambayo amesema ni Bustani ya maua.

Miongoni mwa mambo yaliyowavutia wengi ni uwepo wa Maua mbalimbali ya pekee katika hifadhi,uwepo wa zao la Chikanda ambalo linadaiwa kuwa zao la matajiri na linadaiwa kuchangia nguvu za kiume kwa dhana zilizoko miongoni mwa jamii duniani zinazotumia zao hilo la asili na Matunda poli .

Chikanda ikapata kuulizwa maswali baada ya hifadhi hiyo kueleza inaendelea kupambana na wachimba chikanda katika hifadhi hiyo ambapo mmoja ya waongoza watalii alisema

"Chikanda ni mmea unao toa mfano wa kiazi kimoja na kinatumika kwa chakula umekuwa ukichimbwa sana na watu kwa dhana kuwa unasaidia kuongeza nguvu za kiume na wengine wameweka na dhana kuwa chikana ni chakula cha matajiri"alijibu swali la waandishi wa habari

Waandishi wa habari kutoka mkoa wa Njombe wametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya malazi,sehemu za mapumziko kwa watalii maporomoko ya maji na kuwaona wanyama wengine kama swala jambo ambalo liliwafurahisha wengi katika safari hiyo.

Baada ya safari ya zaidi ya masaa matatu hadi manne katika hifadhi hiyo iliyojaa madhari mazuri na yakuvutia utalii, Kaimu Mhifadhi Mkuu Bw.Jackson Shirima aliwataka waandishi hao kuendelea kuwa mabalozi wa hifadhi hiyo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...