Dar – es – salaam, Tanzania

Adanian Labs ni kampuni  ya kujenga uwezo kwa waafrika yenye lengo la kujenga, kulea na kuzindua kampuni 300 zenye lengo la kuleta athari chanya za kimaendeleo na wajasiriamali wanao fanya kazi kutatua changamoto kubwa zinazowakabili waafrika.  Baada ya siku 30 za tathmini ya kina, kampuni ya Adanian Labs imefanikiwa kuchagua na kutangaza washindi wanne wa programu yake ya kujenga uwezo (Venture building program) kwa mwaka 2022. 

Pichani; Mkurugenzi Mtendaji wa Adanian Labs, Bwana John Kamara akiwa pamoja na washiriki katika siku ya kuonyesha mifano ya kazi (Demo day) tukio lililofanyika katika ofisi za Adanian Labs, jijini Dar es Salaam.

 Programu hii ilipokea maombi kutoka katika sekta mbalimbali katika teknolojia ya Fedha (FinTech), Teknolojia ya Elimu (EduTech), Teknolojia ya Kilimo, (AgriTech) Teknolojia ya Afya (HealthTech), Teknolojia ya Mazingira (EnviroTech), Teknolojia ya Bima (InsurTech), Teknolojia ya Nishati (EnergyTech), Smart-City, MobilityTech, Emmersive tech ikiwemo IOT, Blockchain na AI.

 'Tunapenda kutoa shukurani zetu kwa wajasiriamali wote chipukizi ambao walitutumia maombi na tunawapongeza wote kwa dhana zao zenye kuleta mabadiliko katika jamii na zenye lengo la kutatua changamoto zinazolikumba bara la Afrika' alisema Bwana John Kamara, Mkurugenzi Mtendaji wa Adanian Labs.

Programu ya kujenga uwezo ambayo inatekelezwa na kufadhiliwa na Adanian Labs kwa thamani ya dola 120,000 itakuwa ikifanyika kila mwaka kwa lengo la kusaidia kuwawezesha wajasiriamali chipukizi wa teknolojia wenye mifumo ya awali ambayo inaweza kuendelezwa zaidi.

'Katika kipindi cha miezi kumi na mbili cha programu, washiriki wataweza kupata msaada wa kitaalamu kutoka kwa Adanian Labs, Ushauri wa biashara, kuweza kufikia masoko, ushirika na ufadhili na vile vile kuwasaidia kutumia kanuni Konda (Lean Principle) katika michakato, kujifunza na kuweka makadirio ya uvumbuzi wao' aliongeza bwana John. 

Kampuni ya Adanian Labs ina vituo viwili vya ubora katika AI na Blockchain, AICE Africa (AI Center of Excellence Africa) na The Africa Blockchain Center (The ABC) ambavyo vinakusudiwa kusaidia mkakati wake wa kutimiza mageuzi ya teknolojia Afrika, kujenga uwezo na kuwapa mafunzo wahandisi chipukizi wa teknolojia kuanzisha mifumo ya kiteknolojia kwa kutumia teknolojia ya smart.

Wajasriamali chipukizi wa teknolojia waliochaguliwa kwa programu ya mwaka mzima ni: 

Smart Darasa – Huu ni mfumo shirikishi wa kujifunza  ambao una lengo la kuleta mazingira bora ya kujifunzia kwa kutumia mbinu za ushirikishi za 3D na teknolojia ya AR kwa wanafunzi nchini Tanzania

 

FoundHER Ventures – FoundHER ventures inatumia teknolojia kuweka viwango na kupima sekta zisizo rasmi nchini Tanzania.  Mifumo yao ya masoko ya biashara ya mtandao (e-commerce) inayowezeshwa na mifumo ya SME ERP ina lengo la kuhakiki, kuweka viwango na kupima biashara zinazoongozwa na wanawake Afrika.

 

Bizzyn – Mfumo kamili wa biashara na usimamizi wa fedha  wenye zana kamili kwaajili ya uhasibu, orodha ya mali, malipo ya mishahara, uwasilishaji wa kodi, kuandaa ankara, ufuatiliaji wa akaunti ya benki na uhakiki wa mahesabu ya fedha, usimamizi wa matumizi, kupanga bajeti, uchakataji wa malipo na usimamizi wa akaunti za kupokea na kufanyia malipo.

 Chapaa – Mfumo wa huduma za kifedha kidigitali ambao inakuwezesha kuongeza zaidi thamani ya fedha zako pamoja na jamii inayokuzunguka.

 'Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020, Adanian Labs imeweza kuwalea wajasiriamali chipukizi wa teknolojia bora wapatao kumi na nne (14) katika sekta mbalimbali.  Tunakusudia kujenga kizazi kijacho chenye kuleta athari chanya kwa jamii na makampuni yenye msukumo wa kibiashara ambayo yataleta mabadiliko ulimwenguni kutoka Afrika na programu yetu ya kujenga uwezo itakuwa ni chombo cha uhakika cha kufanya jambo hili kuwa halisi ' alisema.

Washindi walichaguliwa kutoka katika kundi la wajasiriamali chipukizi wapatao 15 ambao kwa makusudi wanatumia teknolojia kuleta masuluhisho na mifumo yenye manufaa.  Kamati ya uhakiki uliundwa na jopo la wadau mbalimbali katika sekta ya wajasiriamali wataalamu wa teknolojia ambao walifanya mahojiano na waombaji waliopendekezwa.

'Tunatazamia katika mfululizo wa miezi 12 ya ushirikano na wajasiriamali wetu waliochaguliwa wenye vipaji kwa matumaini ya kuwapatia msaada unaohitajika kukuza zaidi kazi zao kibiashara na katika ubunifu' alisema bwana John wakati wa kumalizia.

 Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

Zainab Abdallah

Meneja Mawasiliano na Masoko

+255 743 255 628


 

 

 

 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...